Na Ibrahim
Yassin, Tunduma
WAFANYABIASHARA wanaosafirisha
samaki wakavu na dagaa kwenda nje ya nchi kupitia mpaka wa Tunduma
mkoani Mbeya
wametishia kufanya maandamano makubwa ya kupinga kitendo cha Serikali
kuwatoza
ushuru mara mbili katika bidhaa moja.
Wakizungumza na mtandao huu mjini
Tunduma, wafanyabiashara hao wamesema kuwa Halmashauri ya Mamlaka ya Mji
mdogo
wa Tunduma imekuwa ikivunja makubaliano yaliyofikiwa katika vikao vya
pamoja na
kuanza kuwatoza ushuru mara mbili jambo ambalo linasababisha wateja wao
kuwakimbia.
Mmoja wa wafanyabiashara hao,
Kijiko Isagaswa alisema kuwa katika makubaliano baina ya
wafanyabiashara,
Halmashauri na Serikali kuu ni kwamba Bidhaa zote zinazosafirishwa
kwenda nje
ya nchi zinalipiwa kodi Serikali Kuu katika Wizara ya Maliasili na
Utalii na
bidhaa zinazouzwa ndani ya nchi ushuru wake unakusanywa na Halmashauri
ya Mji
mdogo.
Akadai kuwa Halmashauri imekuwa
ikikiuka makubaliano hayo na kutaka ikusanye ushuru hata kwa bidhaa
zinazosafirishwa nje ya nchi, hali ambayo nasababisha kutoelewana na
wafanyabiashara hao, na kusababishwa baadhi yao wasiokubaliana na
kitendo hicho
kukamatwa na kufunguliwa kesi mahakamani.
Isagaswa alisema kuwa tayari
wafanyabiashara wamekaa vikao vya kujadili suala hilo na sasa wameamua
kuonana
na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ili awasaidie kutatua kero hiyo huku wakidai
kuwa kama
jitihada hizo zitashindikana watahamasishana kufanya maandamano makubwa
mjini
Tunduma ili kuishinikiza Serikali iwasikilize.
“Tumeshafanya vikao vingi vya
pamoja kujadili suala hili, hata viongozi wa kutoka taifani wamefika
hapa
tukazungumza na kufikia makubaliano ya Halmashauri ukutojihusisha na
ushuru wa
bidhaa zinazoenda nje ya nchi lakini imekuwa ikikiuka, sasa tumeamua
kuchukua
hatua ya mwisho ya kuonana na Mkuu wa Mkoa na ikishindikana tutaandamana
ili
watusikilize,” alisema Isagaswa.
Mfanyabiashara mwingine, Emmanuel
Almasi alisema kuwa wafanyabiashara wanakerwa na kitendo cha kutozwa
ushuru
mara mbili kwa kuwa kinasababisha bidhaa zao (samaki) wapande bei kiasi
cha
wateja wao kushindwa kumudu na kuhamia maeneo mengine kama vile
Msumbiji,
Mwanza na Zanzibar ambako hawatozwi ushuru mara mbili.
Alisema hali hiyo inasababisha
bidhaa zao kukosa soko na kuwafanya washindwe kumudu maisha sambamba na
kulikosesha taifa mapato halali, kwa kuwa biashara hiyo inakuwa ya kusua
sua.
“Kitendo cha kututoza ushuru mara
mbili kinatuathiri sana kwa sababu bidhaa zetu sasa hazinunuliki na
hivyo
kutufanya tuwe na maisha magumu, lakini hata Serikali yenyewe inakosa
mapato
kwa sababu biashara hii sasa haifanyiki ipasavyo,” alisema Almasi.
Alisema kuwa baada ya
wafanyabiashara kulalamika kwa kufuata sheria na taratibu zote bila
mafanikio,
sasa wako tayari kufanya maandamano ili sauti zao ziweze kusikika kwa
viongozi
wa kitaifa, ambao wanaamini kuwa huwenda hawajui adha zinazowapata.
Chrispine Simwimba alisema kuwa
uvumilivu wa wafanyabiashara dhidi ya manyanyaso ya kukamatwa na
kufunguliwa
kesi bila sababu za msingi sasa umefikia kikomo na wanachotaka sasa ni
kutumia
nguvu ya umma kuieleza Serikali kuwa wamechoshwa na unyanyasaji dhidi
yao.
“Bidhaa
zetu zinakamatwa na
kushikiliwa Polisi kwa muda mrefu bila kujali kuwa zinaharibika na
kutusababishia hasara, sisi wenyewe tunafunguliwa kesi ambazo hazina
hata
ushahidi na hivyo kutupotezea muda wa kwenda mahakani kila wakati, haya
ni
manyanyaso ambayo sasa tunataka uyakomeshje kwa kufanya maandamano
makubwa hapa
Tunduma,” alisema Simwimba.
Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Abbas
Kandoro alipoulizwa kuhusiana na kero ya wafanyabiashara hao alisema
kuwa
maandamano ni haki ya kikatiba ya kila mwananchi hivyo hatishwi na kauli
za
maandamo zinazotolewa na wafanyabiashara hao.
Hata hivyo alisema kuwa Serikali
imeshatoa maelekezo kwa uongozi wa Halmashauri ya Mamlaka ya Mji mdogo
wa
Tunduma kuhusu jinsi ya kushughulikia tatizo hilo na anaamini kuwa
utekelezaji
wa maagizo hao utamaliza tatizo hilo.
“Mamlaka ya mji wa Tunduma
tumeshaipatia maelekezo ya kumaliza tatizo hilo hivyo naamini kuwa
litakwisha
muda si mrefu punde maelekezo yaliyotolewa yatakapoanza kufanyiwa kazi,”
alisema Kandoro.
Sakata la wafanyabiashara hao
kutozwa ushuru mara mbili liliwahi kufikishwa kwa Mlezi wa Chama Cha
Mapinduzi
Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Waziri wa Ulizi na Usalama, Shamsi Vuai
Nahodha alipofanya
ziara ya kichama mkoani hapa hivi karibuni ambaye pia aliagiza
Halmashauri ya
Mamlaka ya Mji mdogo wa Tunduma kufuata sheria ambayo inaelekeza kuwa
bidhaa
zinazosafirishwa nje ya nchi zitozwe kodi Serikali Kuu na zile
zinazouzwa ndani
ya nchi ushuru wake ukusanywe na Halmashauri.
