![]() |
| Taswira ya stendi kuu Masasi leo. |
Baada ya kufuatilia kwa undani, na kwa
upana kuhusu swala la gesi ambalo linaendelea kuwa ni mgongano au, ni
mgogoro
kati ya Serikali na wananchi wa Mkoa wa Mtwara/Lindi kuhusu ujenzi wa
bomba la
kusafirisha gesi kwenda kinyerezi Dar- es –Salaam, tumebaini yafuatayo:-
1. Hakuna Sera ya gesi ambayo
husababisha kupatikana Sheria baada ya kupelekwa Bungeni na kuidhinishwa
bali
kilichopo ni rasimu ya sera ambayo haina ushirikishwaji wa mawazo ya
wananchi
wa Mkoa wa Mtwara na Lindi, ambako vyanzo vya gesi hiyo ipo.
2. Elimu kuhusu gesi na manufaa yake kwa
wananchi haikutolewa ili kujua haki zao kwa madhara yatokanayo na
(Uvunaji)
uzalishaji wa gesi hiyo,
na jinsi watakavyonufaika.
Chama cha Mapinduzi katika Ilani yake ya
uchaguzi ya mwaka 2010 inatamka wazi katika Ibara ya 63 kifungu cha H na
K juu
ya gesi ya Mnazibay Mtwara na Songo songo Kilwa, Lindi kuhusu umeme wa (240 MW)
Kinyerezi na (300MW) Umeme wa Mnazi bay Mtwara……
-Vifungu hivi vinafafanua:
• Gesi ya Mnazi bay itakuwa kwa ajili ya
Mitambo ya kuzalisha umeme ambayo itajengwa Mtwara (300MW)
• Mitambo ya kuchakata gesi kujengwa Mtwara
• Ujenzi wa viwanda Mtwara ili malighafi
itokanayo na gesi itumike kutengeneza mbolea, plastic
vikiwemo na viwanda vya
Cementi
2. Gesi ya Songo songo inafafanua wazi
kuwa gesi hiyo itapelekwa Kinyerezi . Dar –es –Salaam kwa madhumuni hayo
hayo.
• Kuendeleza viwanda mbali mbali
• Kuzalisha umeme (240 MW)
• Kuchakata gesi kwa kujenga mitambo
Katika ahadi ya Rais wa Jahuri ya
Muungano wa Tanzania alizotoa wakati wa Kampeni za uchaguzi katika hotuba yake
ya tarehe 29/10/2010 alitamka wazi kuwa Mkoa wa Mtwara uwe tayari kwa
maendeleo
makubwa ambayo yanakuja kutokana na gesi iliyogunduliwa katika Mkoa wa
Mtwara huko Mnazi bay
Alimainisha/aliainisha juu ya viwanda
mbalimbali vitakavyojengwa hapa mkoani vya mbolea,cement, plastic n.k na
kuwataka wananchi wajiandae kupokea maendeleo hayo kwa kujenga nyumba
nzuri zenye sifa kwa ajili ya wageni. Pia wawasomeshe
watoto wao ili wawe na elimu ya
juu na kupata ajira katika Makampuni yanayokuja.
BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI>>>>>>>>>
BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI>>>>>>>>>
