![]() |
| Andrew Chenge. |
Chenge ambaye ni mbunge wa Bariadi Magharibi ameongeza kuwa
mgombea huyo lazima adhibitiwe katika masuala mbalimbali yakiwamo ya
dini na mengineyo.
Akitoa mapendekezo yake jana mbele ya Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, alisema iwapo sasa mgombea wa chama cha siasa ana sheria na
taratibu zinazomdhibiti lazima binafsi naye adhibitiwe.
Chenge pia alipendekeza Rais asipunguzwe madaraka isipokuwa katika
kuteua watendaji uwepo uthibitisho.
Akizungumzia kumpunguzia madaraka Rais alisema kuna miundo miwili
ya utawala ya Waziri Mkuu kuwa mtendaji au Rais kuwa mtendaji lakini
nchini Rais ni mtendaji lakini anasaidiwa na tume mbalimbali hivyo la
msingi labda katika uteuzi akishateua watu wathibitishwe.
Akizungumzia maadili alipendekeza Sekretarieti ya Maadili ya umma
iwe tume ya kikatiba ili iwe na meno kwa kuwa na viongozi weledi na
wenye uzoefu.
Alisema hata kama tume hiyo haitakuwa na meno ya kuwafikisha
mahakamani viongozi watakaokiuka maadili wawe na uwezo wa kufikisha kwa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili wachukuliwe hatua.
Hivyo alitaka Tume iwe na uwezo kwa kupatiwa rasilimali za kutosha
na watendaji wenye weledi katika kusimamia maadili yakiwamo ya rushwa.
Hata hivyo alisema Chenge alisema katika Katiba haiwezekani kuzungumzia
rushwa bali ni kujenga misingi itakayosaidia kuidhibiti kwa kutungwa
sheria.
