Serikali Iache Kutafuta Mchawi, Iende Mtwara – Zitto
KATIKA kipindi cha wiki nne sasa kumekuwa na maandamamo, malumbano na
vurugu kuhusu mradi wa kujenga bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka
Mtwara hadi Dar es Salaam. Mradi huu wa kutandaza bomba la urefu wa
kilometa 542 ni mkubwa sana hapa nchini, na una thamani kubwa zaidi
kuliko miradi mingine yote ya miundombinu iliyopata kutokea hapa nchini.
Mradi huu utajengwa kwa mkopo wa dola za Kimarekani 1.2 bilioni kutoka
Benki ya Exim ya China.
Wananchi wa Mtwara kupitia maandamano ya tarehe 27 Desemba 2012
wametaka kujua hatma ya maendeleo ya mikoa wa kusini kutokana na mradi
huu wa bomba la gesi. Serikali imewajibu wananchi hawa kwa kuwaita
wahaini, watu hatari na wasio elewa. Imefika mahali inapotosha madai yao
kwamba hawataki gesi itoke Mtwara.
Kimsingi Serikali haijajibu hoja yeyote ya msingi ya wananchi wa
Mtwara kuhusu mradi wa kusafirisha gesi. Badala yake imekuwa ikijaribu
kupotosha madai ya watu wa Mtwara kupitia mikutano na vyombo vya habari.
Tangu maandamano haya yatokee, na baadaye mikutano ya hadhara na
hatimaye matukio ya kusikitisha ya kuharibu mali za watu, mauaji ya
watu na majeruhi mbalimbli, Serikali na hasa Wizara yenye dhamana ya
mradi huu, imekuwa ikitoa matamko kwenye vyombo vya habari badala ya
kwenda Mtwara kuzungumza na wananchi, kusikiliza madai yao na kuona
namna ya kutekeleza madai hayo. Kutokana na Serikali kutofanya hivyo,
hatimaye matukio ya kusikitisha ya kuharibu mali za watu, mauaji ya
watu na majeruhi mbalimbli, Serikali na hasa Wizara yenye dhamana ya
mradi huu, imekuwa ikitoa matamko kwenye vyombo vya habari badala ya
kwenda Mtwara kuzungumza na wananchi, kusikiliza madai yao na kuona
namna ya kutekeleza madai hayo. Kutokana na Serikali kutofanya hivyo,
kusikiliza na kuzungumza na wananchi wa Mtwara, vurugu mbaya sana zimeendelea mkoani humo.
Mwezi uliopita, Desemba 2012, tatizo lilionekana kuwa ndogo na lenye
kuhusiana zaidi na ukosefu wa kushirikishwa kwa wananchi. Badala ya
kushughulikia
tatizo likiwa bado ndogo, Serikali imeona njia pekee ya kushughulikia suala hili ni kutafuta mchawi na kwa wiki zote hizi imekuwa ikisemakuwa wanasiasa na makampuni ya uwekezaji ya nje yanachochea mgogoro
huu.
tatizo likiwa bado ndogo, Serikali imeona njia pekee ya kushughulikia suala hili ni kutafuta mchawi na kwa wiki zote hizi imekuwa ikisemakuwa wanasiasa na makampuni ya uwekezaji ya nje yanachochea mgogoro
huu.
Leo hali iliyopo mkoani Mtwara inasikitisha sana, maana mali za
wananchi zinaharibiwa, nyumba zinachomwa moto na watu wanapoteza maisha.
Tunalaani matukio haya kwa nguvu zetu zote, maana kinachotokea Mtwara
si Utanzania. Tusipowasikiliza wananchi na kutatua mgogoro huu kwa
kuwashirikisha, hali itazidi kuzorota wakati tukitupiana lawama.
Hivi sasa serikali imeona njia pekee ya kushughulikia suala hili ni
kutafuta mchawi na kwa wiki zote hizi imekuwa ikisema kuwa wanasiasa na
makampuni ya uwekezaji ya nje yanachochea mgogoro huu.
Kwanza, Serikali imekuwa ikiaminisha umma kwanza suala hili
limechukuliwa kisiasa. Pili, Serikali imekuwa ikirudia kusema kuwa
baadhi ya makampuni ya uwekezaji nchini na mataifa ya Magharibi yamekuwa
yakichochea wananchi wa Mtwara.
Katika mwendelezo wa mtindo wa Serikali wa ‘management by press
conferences’ jana Jumamosi Naibu Waziri wa Nishati na Madini ndugu
George Simbachawene aliwaambia wahariri kwamba mimi Zitto Kabwe
ninachochea wananchi wa Mtwara, ninatumiwa, na si mzalendo. Vile vile
alitoa vielelezo kadhaa kuonyesha kuwa mradi wa kujenga bomba la gesi ni
gharama sawasawa. Akasisitiza kwamba mimi ni mwongo.
Katika kipindi chote cha mgogoro wa Gesi Mtwara, sijafika Mtwara.
Sijafanya mkutano wowote na waandishi zaidi ya kuandika mawazo yangu,
kama Mtanzania kuhusu suala hili.
Nimeandika makala nne na zimechapishwa katika magazeti kadhaa hapa
nchini na kwenye blogu yangu (http://zittokabwe.wordpress.com/).
Niliandika: Utajiri wa Gesi Asilia: Tuwasikilize Watanzania wa Mtwara
na Lindi. Nikaandika tena: Tusipuuze mandamano dhidi ya Bomba la Gesi:
Kilio cha Uwajibikaji; Nikaandika tena: Mtwara : Serikali inavunja nchi
kwa kutosikiliza Wananchi; ni baadhi ya makala nilizoandika kuhusiana na
suala la Mtwara.
Sitaki kubishana na Naibu Waziri ama Kiongozi yeyote ya Serikali kwa
sasa. Hatuwezi kuendelea kulumbana, kuzozana, kuzodoana na kurushiana
maneno wakati nchi yetu inaungua. Huu sio wakati wa kutafuta mchawi bali
kutafuta majawabu ya changamoto zilizopo mbele yetu.
Yanayotokea Mtwara ni fundisho kwetu kwa Taifa namna ya kukabili
changamoto za utajiri wa rasilimali, ili kuweka mkakati, mambo haya
yanayotokea Mtwara yasitokee tena Tanzania. Tutaweza kuzuia maafa haya
iwapo tutaweka uwazi katika mikataba, tutashirikisha wananchi kwenye
unyonyaji wa maliasili za nchi, na iwapo tutaweka uwajibikaji.
Rais Kikwete Kikwete ana majibu; ayatoe sasa kwa wana Mtwara
Kwa mujibu wa Mpango Kabambe wa Umeme nchini (Power System Master
Plan), kulikuwa na mradi wa kufua umeme MnaziBay, ambao Rais Jakaya
Kikwete aliagiza utekelezwe mara moja. Serikali ieleze umma kuhusu mradi
huo wa kujenga kituo cha kufua umeme 300MW MnaziBay Mtwara na kujenga
msongo wa umeme wa 300KV mpaka Singida. Umeishia wapi? Ikumbukwe kuwa
mnamo tarehe 12 Oktoba 2012,
Rais Jakaya Kikwete alipokea ripoti ya
ujenzi wa mradi huu kutoka makampuni ya China National Machinery &
Equipment Import & Export Corporation (CMEC) ya China na Siemens ya
Ujerumani, ambayo kwa pamoja yalitarajia kujenga kituo kikubwa cha
kuzalisha umeme kutokana na gesi katika eneo la Mnazi Bay, mjini Mtwara
na pia kujenga njia ya kusafirisha umeme ya kilomita 1,100 kutoka Mtwara
hadi Singida. Mradi huu ungegarimu dola za kimarekani milioni 684 na
Rais aliagiza utekelezwe haraka sana. Huu mradi uliishia wapi? Kwa nini
Serikali ipo kimya kuhusu mradi huu ambao ungejibu kabisa maswali ya
watu wa Mtwara? Taarifa ya Ikulu kuhusu mradi huu imeambatanishwa hapa.
Tufanyeje?
Hapa tulipofikia ni lazima kwanza kabisa kusikia kilio cha wananchi
wa Mtwara ikiwemo kuelewa madai yao. Swali kubwa kubwa la watu wa Mtwara
na Kusini kwa ujumla ni ‘tunanufaikaje’? Jibu la swali hili si ahadi za
miradi bali ni vitendo. Hapa ndipo serikali inaposhindwa kushughulikia
suala hili, kutoelewa madai ya wananchi na kuyapotosha.Viongozi wa
kisiasa wenye ushawishi kutoka pande zote, chama tawala na vyama vya
upinzani, waende Mtwara kuzungumza na wananchi, lakini wawasikilize
kwanza.
1. Lazima viongozi tujenge utamaduni wa kusikiliza wananchi na si
kuwahutubia tu. Wananchi wa Mtwara wana madai ambayo lazima viongozi
tukae kitako kuwasikiliza kisha kufanya nao majadiliano ambayo yatatoa
mwafaka. Rais mstaafu, Ndugu Benjamin Mkapa ameshatoa kauli kuhusu suala
hili. Ni wakati mwafaka sasa kwa viogozi wengine kumuunga mkono kwa
kwenda Mtwara na kukaa na wananchi wa Wilaya zote za Mtwara, kusikiliza
hoja zao na kuona namna ya kupata ufumbuzi wa suala hili. Wakati hatua
hii inachukuliwa, wananchi waombwe kutulia na kuacha vurugu za aina
yeyote ile, na Serikali isimamishe mradi mpaka hapo suluhu na wananchi
itakapopatikana.
2. Wakati juhudi hizo zinaendelea Serikali iweke wazi mkataba wa
ujenzi wa bomba, kwani ni dhahiri gharama za mradi huu ni kubwa mno
kulingana na uhalisia wa miradi ya namna hii duniani kote. Katika
taarifa zote kwa umma Serikali imekuwa ikisema kwamba mradi utagharimu
jumla ya dola za kimarekani 1.2 bilioni, lakini katika taarifa ambayo
Wizara ya Nishati na Madini imesambaza jana kwa wahariri wa vyombo vya
habari nchini imesema mradi utagharimu dola za kimarekani milioni 875.
Usiri katika mkataba huu unaashiria kwamba Serikali inaficha kitu. Hivyo
njia pekee ni kutaka mkataba uwe wazi kwa wananchi.
3. Wakati tunawataka wananchi wa Mtwara kuruhusu utulivu, ni vema
Serikali ijiandae kutoa majawabu ya madai ya wananchi hao. Majawabu ya
Serikali yajikite kueleza wananchi wa Mtwara wanafaidikaje na rasilimali
ya gesi asilia kwa maendeleo yao. Wananchi wa Mtwara wanataka
uwajibikaji wa Serikali kwenye utajiri wa nchi, na wamechoka na porojo
za orodha ya miradi isiyotekelezwa.
Viongozi twendeni Mtwara kusikiliza wananchi wetu. Nchi inaungua na
hatuwezi kuendelea kuzozana badala ya kuzima moto huu hatari kama vita
vya MajiMaji. Mimi nakwenda Mtwara haraka na mara baada ya viongozi
wangu wa chama kutoa ridhaa.
ZITTO KABWE
Mbunge, Kigoma Mjini (Chadema)
Waziri Kivuli wa Fedha
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni
Mbunge, Kigoma Mjini (Chadema)
Waziri Kivuli wa Fedha
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni