Mwenyekiti wa kitongoji cha Mowalak
kijiji cha Sukuro wilayani Simanjiro mkoani Manyara,Lengai Ole Makoo
akilaani kitendo cha baadhi ya viongozi wa serikali na kisiasa wilayani
humo kwa kuwakamata hovyo na kisha kuwabambikia kesi baadhi ya viongozi
wa kijiji hicho juzi katika mkutano ulioitishwa na serikali ya kijiji
hicho,kushoto kwake ni mwenyekiti wa kitongoji hicho,Kaayai Murero(picha
na habari na Jamii blog http://pamelamollel.wordpress.com
WANANCHI wa kijiji cha
Sukuro wilayani Simanjiro mkoani Manyara wamemwomba Rais Jakaya Kikwete
aingilie kati sakata la mpaka kati ya kijiji chao na Kitiengare kilicho
dumu kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi huku wakisema kuwa wamechoka
kunyanyaswa kwa kukamatwa mara kwa mara na kisha kubambikiwa kesi
mbalimbali viongozi wao jambo ambalo linapelekea wao kukosa maendeleo
Pia,wamemtupia
lawama mbunge wa jimbo hilo Christopher Ole Sendeka kwa kutowasaidia
katika mgogoro huo sanjari na kusikitishwa na kauli zake kwamba mgogoro
huo umeshamalizika huku wakidai nijambo ambali halijapatiwa ufumbuzi
bado
Wakizungumza kwa
nyakati tofauti katika mkutano ulioitishwa na uongozi wa serikali ya
kijiji hicho kujadili tukio la kukamatwa kwa viongozi wa serikali ya
kijiji hicho pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi hivi karibuni
walionyesha kutoridhishwa na viongozi wa serikali Mkoani hapo“Hatuna imani na viongozi wetu wa
serikali pamoja na mbunge wetu,,,tumeendelea kunyanyaswa hadi kufikia
kukamatwa kwa viongozi wetu wa kijiji jambo ambalo limezidi kukutesa
sana hapa kijijini”sauti ilisikika katika mkutano huo
Akizungumza katika
mkutano huo,mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho,Kaayai Murero
alisema kwamba hivi karibuni baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji
hicho akiwemo yeye pamoja na viongozi wa chama cha Mapinduzi(CCM)
walikamatwa na jeshi la polisi na kisha kuachiwa katika mazingira ya
kutatanisha.
Alisema kuwa
kumekuwa na hali ya wasiwasi kijijini kwao kwa kuwa baadhi ya familia
zinaishi kwa hofu kutokana na mgogoro wa ardhi baina ya kijiji chao na
Kitiengare kwa kuwa wamekuwa wakikamatwa hovyo na jeshi la polisi
wilayani humo na kisha kubambikiwa kesi.
Mwenyekiti huyo kwa
unyonge alimuomba Rais Kikwete kuingilia kati mgogoro huo huku akidai
kuwa umedumu kwa muda mrefu na uongozi wa serikali na chama cha CCM
mkoani Manyara hauonyeshi jitihada za dhati kuutatua mgogoro huo.
Naye,mwenyekiti wa
kitongoji cha Molawak,Lengai Ole Makoo alisema kuwa baadhi ya wananchi
waekuwa wakikamatwa hovyo na jeshi la polisi kwa madai ya kuchangia
fedha za kuendesha kesi iliyopo mahakamani kwa lengo la kudhoofishwa ili
wasipate mwanya wa kuendelea na kesi hiyo
Alisema kuwa
wananchi hao wamekuwa wakipigwa na kutishiwa kunyang”anywa kadi za CCM
kwa madai kwamba waachane na kesi ya kudai ardhi waliyoifungua
mahakamani wilayani Babati na kumtaka Rais Kikwete aingilie kati.
Nao baadhi ya wakazi
wa kijiji hicho,Abraham Koringo,Olais Soyai na Magdalena Daniel
walimwomba Rais Kikwete kuwasaidia katika unyanyasaji huo huku wakidai
kwamba wamekuwa wakihangaishwa kwa muda mrefu kama wao ni wakimbizi
katika nchi yao
Hata hivyo
walisisitiza kwamba baadhi ya wanasiasa pamoja na viongozi wa serikali
hawana nia njema ya kuutatua mgogoro huo uliodumu kwa takribani miaka
mitano kwa kuwa wananufaika kwa kupokea chochote.
“Tunaitaka serikali
ifanye maamuzi magumu tunamwomba mheshimiwa Rais aingilie kati kwa kuwa
vijiji vya Kitiengare na Sukuro vilitenganishwa kisheria sasa hii leo
tunataka kunyang”anywa ardhi yetu”walisema kwa unyonge wananchi hao
Pia Katika mkutano
huo baadhi ya wazee wa mila maarufu kama Malaigwanani walihudhuria
mkutano huo ambapo kwa sauti ya pamoja walitoa tamko la kuendelea
kuchangishana fedha za kugharamia kesi waliyoifungua mahakamani kudai
ardhi ndani ya kijiji chao.