RAIS
wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
(pichani) anaanza ziara rasmi ya Kiserikali nchini Ufaransa leo,
Jumamosi, Januari 19, 2013, kwa mwaliko wa Rais wa Ufaransa, Mheshimiwa
Francois Hollande.
Rais Kikwete na ujumbe wake aliondoka nchini usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uswisi kuelekea Ulaya kwa ajili ya ziara hiyo.
Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja waNdege wa Charles De Gaul mjini Paris leo jioni, Rais Kikwete ambaye anafuatana na Mama Salma Kikwete atapokelewa rasmi katika Ufaransa kwa gwaride na kupokelewa na Waziri wa Misaada ya Maendeleo wa Ufaransa, Mheshimiwa Paschal Canfin.