Mkurugenzi, na mwanamuziki wa East
African Melody Modern Taarab, Lamania Shaaban amefarika usiku wa kuamkia
leo akiwa usingizini. Lamania alikuwa mpiga gitaa na mtunzi mzuri wa
muziki wa Taarab, na atakumbukwa kwa tungo zake kama 'Utalijua Jiji'.
Marehemu alianza kuugua kiasai cha
miaka minne iliyopita baada ya kupata stroke iliyomuweka kitandani kwa
muda mrefu sana, karibuni alianza kuwa na nafuu kiasi cha kuweza
kuhudhuria Ibada kwenye Msikiti uliokuwa karibu na kwake. Lakini Mungu
amempenda zaidi na amefariki leo.
Marehemu atazikwa Tandika Maguruwe,
baada ya Ibada za mwisho katika Msikiti wa Sheikh Kilembe kesho saa 7
mchana. Msiba uko Tandika Maguruwe, Mtaa wa Muwale. Habari na http://musicintanzania.blogspot.com/