Wahariri na
Waandishi wa Habari zaidi ya 40 wameshiriki kwenye semina kuhusu Kanuni
za
Uchaguzi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyofanyika leo
(Januari 16 mwaka huu).
Wawezeshaji
katika semina hiyo iliyofanyika ofisi za TFF walikuwa Kamati ya Uchaguzi
ya TFF
iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Deogratias Lyato na Katibu Mkuu wa TFF,
Angetile Osiah. Pichani anayezungumza ni Lyato katikati, kushoto Osiah
na kulia Hamidu Mbwezeleni, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
|