Na
Elizabeth John
SHIRIKISHO la
Filamu Tanzania (TAFF) limekemea baadhi ya
wasanii walioonyesha utovu wa nidhamu katika msiba wa aliyekuwa msanii
wa filamu nchini, Juma Kilowoko
‘Sajuki’.
Pia limesisitiza
kuwa msanii atakaeripotiwa katika vyombo
vya habari kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu atafungiwa kuigiza.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Rais wa TAFF,
Simon Mwakifwamba alisema amesikitishwa na kitendo cha wasanii kuacha
msiba na
kwenda kunywa pombe wakati msiba huo ni wa dini.
Alisema baadhi
ya wasanii kuonyesha utovu wa nidhamu
katika msiba wa marehemu Kanumba na wengine katika msiba wa Sajuki.
“Nasikitika
kuona msanii hajitambui hata kidogo, yani
anaacha msiba anakwenda kunywa pombe tena jirani na mahala pa msiba,
jamani huu
msiba ni wa dini, hivyo atakayeripotiwa vibaya katika misiba TAFF
tutamfungia”
alisema Mwakifwamba.
Katika hatua
nyingine alisema msiba huo ulitawaliwa na
utani hali ya kwamba umewakutanisha watani wa makabila.
Msiba huo
ulitawaliwa na utani baada ya kuwepo kwa
wasanii wachekeshaji kama vile, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ ambaye ni
mwenyekiti wa kamati ya fedha, Lucas Mhuvile ‘Joti’ na wengineo wengi.