MAKAMU WA RAIS DKT.GHARIB BILAL AENDESHA KIKAO CHA MUUNGANO MJINI ZANZIBAR LEO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiendesha Kikao cha Muungano, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo, Januari 14, 2013. Wa pili (kushoto) ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (wa pili (kulia) Ni Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kushoto) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samiah Suluhu na (kulia) ni Waziri wa nchi Ofsi ya Makamu wa pili wa Rais zanzibar, Mohamed Aboud.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Makamu wa pili wa Rais, Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, wakati Makamu alipokuwa akiendesha Kikao cha Muungano kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo, Januari 14, 2013.
Baadhi ya Mawaziri wakiwa ukumbini humo wakati wakifuatilia kikao hicho cha Muumgano kilichoendeshwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (hayupo pichani), leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula (kulia) Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava (katikati) na Mkurugenzi wa Muungano, Rajab Baraka (kushoto) wakifuatilia vifungu katika machapisho ya kujadili masuala ya Muungano, wakati wa kikao cha Muungano, kilichoendeshwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (hayupo pichani), kilichofanyika leo Januari 14, 2013, katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo