



---
Q Chilla amesema kuingia kwake kwenye
matumizi ya
madawa ya
kulevya ilisababishwa na baadhi ya watu kuchangia kumrudisha chini na
kujikuta
yuko peke yake katika mitihani aliyokuwa akipitia. Huku akikataa
kuwataja kwa
majina alisema watu hao walihakikisha kila anachokifanya hakifanikiwi
na
kujikuta katika wakati mgumu.
Akiongea na Fina Mango kwenye kipindi cha
Makutano, Qchilla amesema alishindwa kujua amemkosea nani au nani
amuombe
msamaha. Hata hivyo anasema anawashukuru watu wake karibu waliokuwa
wakisikitishwa na hali aliyokuwa nayo na kuamua kumshauri aache kutumia
madawa
hayo. Alipoulizwa anawashauri vipi wasanii ambao wametumbukia kwenye
matumizi
hayo alisema njia pekee ni kukubali kuwa wana tatizo na kuishika dini.
Pia
aliipongeza hatua ya rais Kikwete kumsaidia Ray C ambaye pia alikuwa
aliingia
katika wimbi hilo akitolea mfano wa rais Nelson Mandela aliejaribu
kumsaidia
mwanamuziki Brenda Fassie na Rais Obama aliemsaidia marehemu Whitney
Houston na
kusisitiza wasanii wote ambao ni waathirika wa madawa ya kulevya
kujitokeza ili
wasaidiwe na jamii.
QChilla amesema kwa sasa anafanya muziki
akilenga
soko la
kimatafifa zaidi akiwatolea mfano PSquare na kusema tatizo la
wanamuziki wengi
kuishia kusikika nchini tu ni kujiwekea mipaka na kulenga soko la ndani
tu na
kumalizia hana mpango wa kutoa album badala yake ataendelea kutoa
nyimbo kali.