KINANA, MIGIRO, NAPE WAKAGUA UJENZI WA DARAJA LA KIKWETE MTO MALAGARASI LEO


Wajumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi  (CCM) wakiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana leo walitembelea na kukagua ujenzi wa Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi lililopo wilayani Uvinza Mkoani Kigoma.

Ziara hiyo ya Wajumbe hao ni moja ya shamra shamra za maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM ambayo mwaka huu inaadhimishwa Mkoani Kigoma kitaifa, na Wajumbe hao wameamua kukagua miradi kadhaa ya Maendeleo ambayo iliahidiwa na Chama hicho tawala wakati wa Kampeni zake za Uchaguzi mwaka 2010.

Katika ziara hiyo Kinana ameambatana na Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa UVCCM taifa,Martin Shigela.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo