Mgambo wa jiji la Dar es Salaam
akitekeleza majukumu yake leo, ya kulifunga mnyororo gari lenye namba za
usajili T 569 BHD lililokuwa limepaki vibaya pembeni mwa barabara
maeneo ya feli jijini Dar es Salaam.
Akijiweka sawa mara baada ya kumaliza kufunga.
Huyu dereva aliamua kulipaki gari lake kwa staili hii na kuamua kuondoka bila kutoa maagizo yeyote.
Baada
ya kuwa amelifunga mgambo huyo wa jiji la Dar akichukua kalamu yake na
kuanza kuandika dondoo muhimu. Mgambo huyo baada ya mtandao huu kunyaka
akifanya tukio hili, Ulifanya nae mahojiano nae machache juu ya kazi
hiyo aliyofanya na alisema kuwa wanapomaliza kufunga huwa wanamsubiri
mwenye gari mpaka anapokuja na kuandikiwa faini ya Tsh. 80,000/- kwa
kitendo chake cha kupaki sehemu isiyo rasmi (Picha na habari na matukio)



