DKT SHEIN ASHIRIKI UZINDUZI WA MRADI WA "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA"

   Baadhi ya Watoto wakibeba mabango yenye ujumbe tofauti unaosisitiza kulindwa haki zao,wakipita kwa maandamano mbele ya Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika sherehe za  uzinduzi wa Mradi wa  "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA", zilizofanyika jana katika Uwanja wa Amaan Studiuam,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwapungia Mkono Vijana waliopita mbele ya Jukwaa la Uwanja wa Amaan Studiuam,akipokea maandamano ya vijana katika sherehe za  uzinduzi wa Mradi wa  "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA", ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) ni Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na MIchezo Said Ali Mbarouk
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi zawadi Mwakilishi wa Shirika la UNICEF Paulo Edwards, katika sherehe za uzinduzi wa Mradi wa ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA" ,katika  Uwanja wa Amaan Studium, ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea 

kitabu kutoka kwa Nasra Sheikh Mohamed,wa Skuli ya Mwembeshauri Mjini Unguja,kitabu  

chenye Agenda ya Watoto kuhusu usisitizaji kwa Serikali na Jamii kushirikiana

 katika kuwapatia haki zao za Msingi bila unyanyasaji. katika uzinduzi wa Mradi wa  "ONE 

WORLD FOOTBALL FOR AFRICA",katika uwanja wa Amaan Studium ikiwa ni shamra

 shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitia saini Mpira katika uzinduzi wa Mradi wa  "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA",mradi ambao utawapatia vijana wa Zanzibar Mipira Ishirini Elfu ,(20,000) katika vikundi mbali mbali na kupelekea kuongezeka kwa vipaji vya Soka nchini,katika sherhe za kuadhimisha miaka 49 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo