Mwili wa kijana
huyo ukitolewa
Kijana anayesadikika kuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya (teja) mjini
Iringa Stan Mhepelwa mkazi wa Ilala katika Manispaa ya Iringa amekutwa
akiwa amekufa katika nyumba ambayo bado kukamilika eneo la barabara
mbili katika Manispaa ya Iringa.
Mashuhuda wa tukio hilo wameueleza mtandao huu kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo jumapili ambapo
mwili wa kijana huyo umekutwa mida ya saa 3 asubuhi na wananchi
waliokuwa wakipita eneo hilo .
Samson Kalinga ni mkazi wa eneo hilo amesema kuwa nyumba hiyo
imekuwa ikitumiwa na vijana hao mateja kama sehemu ya kujificha na
kujidunga madawa ya kulevya kwa kutumia sindano na kuwa chanzo cha
kifo cha kijana huyo kinasadikika kuwa alijidunga sindano vibaya .
Hata hivyo alisema mwili wa kijana huyo umekutwa katika chumba
hicho huku pembeni kukiwa na mabomba ya sindano na kuwa aliyetoa siri
ya kifo cha kijana huyo ni teja mwenzake ambae alikuwa akiingia
katika chumba hicho ili kuendelea kutumia madawa ya kulevya.
|