Waziri Kagasheki akiwa mojawapo ya sehemu zenye mgogoro wilayani Mufindi
Wavunaji wadogo wakimsikiliza Waziri Kagasheki.
Waziri Kagasheki akizungumza na wavunaji wadogo wa Sao hii.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Tarehe 27 Januari 2013
Wavunaji wadogo wakimsikiliza Waziri Kagasheki.
Waziri Kagasheki akizungumza na wavunaji wadogo wa Sao hii.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA
MALIASILI NA UTALII
TAARIFA
KWA UMMA
Utangulizi
Waziri wa
Maliasili na Utalii Mhe Khamis Kagasheki amesema kuwa Wizara yake
inathamini sana
mchango mkubwa unaotolewa na wananchi wanaoishi katika vijiji
vinavyozunguka
Shamba la Miti Sao Hill na kuwa Wizara itahakikisha kuwa wananchi hao
wanaendelea
kufaidi matunda yanayotokana na shamba hilo ili waendelee kushiriki
katika
kulitunza.
Waziri Kagasheki
alisema pia kuwa sheria na busara sharti itumike katika kutatua migogoro
ya
uvamizi katika shamba la miti Saohill.
Mheshimiwa
Kagasheki aliyasema hayo katika nyakati tofauti alipotembelea Wilaya ya
Mufindi
Mkoani Iringa juzi Ijumaa na jana Jumamosi tarehe 26 Januari 2013 kwa
nia ya kusikiliza
kero zilizopo wilayani humo kuhusiana na Shamba la miti la Saohill.
Akiwa huko alifanya
mikutano na uongozi wa Mkoa wa Iringa, uongozi
wa Wilaya ya Mufindi, watumishi wa Shamba la miti Saohill Madiwani wa
Wilaya
Mufindi na Wavunaji wa Wadogo wa Miti katika shamba la Saohill.
Katika mikutano
yote alijulishwa kuwa kuna kero mbili kubwa zinazolihusisha shamba la
miti
Saohill. Kwanza ni mgawo wa miti ya kupasua mbao kutoka katika shamba
hilo
ambao ulielezwa kuwa kwa mwaka 2012/13 haukuridhisha.
Pili ni kero ya wananchi
kukosa ardhi ya kulima na kupanda miti kwa kuwa wameongezeka, hivyo
wamevamia
sehemu ya Shamba la Saohill na kulima mazao ya chakula pamoja na kupanda
miti
yao.
Kamati ya Mgawo
Akizungumza na
watumishi wa Shamba la Miti Saohill Waziri Kagasheki alisema kuwa baada
ya
kusoma na kuitafakari taarifa ya ugawaji atawachukulia hatua waliohusika
na mgawo
wa mwaka 2012/13 hususan, Meneja wa Shamba aliyekuwepo wakati wa mgawo
huo na Msaidizi wake, pamoja na mameneja wa tarafa
za shamba la Saohill. Hatua hizo zitakuwa pamoja na kuwasimamisha kazi
ili
wapishe uchunguzi kuhusu mgawo ulivyofanyika. Kwa sasa mamemeja hao
wamehamishiwa vituo vingine.
Vibali vya Uvunaji
Katika mkutano wa
Waziri Kagasheki na wavunaji wadogo, wavunaji hao walimwambia Waziri
kuwa utaratibu
wa uvunaji kwa mwaka 2012/13 ulikuwa
mbovu kwa kuwa kulikuwa na kigezo cha kuwa na mashine ya kuchana mbao
kwanza
ndipo mwombaji afikiriwe kupewa malighafi.
Wavunaji walisema
kuwa , ili kukidhi kigezo hicho, walinunua mashine, wengine kwa mkopo,
lakini
baadhi yao hawakupewa mgawo. Walilalamika pia kuwa baadhi ya wale
waliopata
mgawo waliamua kuuza mgawo wao kwa wenye mashine maana wao hawakuwa
nazo.
Hata hivyo, katika katika kikao hicho, wadau wengine, kama
vile chama cha kupasua mbao cha SAFIA, walisema
wanaridhika na utaratibu mpya wa mgawo uliowekwa na Wakala wa Huduna za
Misitu
(TFS) ambao nia yake ni kukomesha biashara ya ulanguzi katika biashara
ya mbao.
Kuhusu ugawaji
wa miti ya kupasua mbao kwa wadau, Waziri Kagasheki alikubaliana na
malalamiko
ya wavunaji wadogo, kuwa utaratibu uliotumika katika kugawa miti mwaka
2012/13 haukuwa
mzuri na usingeweza kutenda haki maana wajumbe wa Kamati ya Ugawaji ni
Meneja
na wasaidizi wake. Alisema haiwezekani watu wanaohusika na kuuendeleza
na
kuutunza msitu huo kutenda haki wakati wa kugawa mazao.
Waziri Kagasheki
aliahidi kuwa ataiunda upya Kamati ya mgawo wa miti ya kuvuna katika
Shamba la
Saohill. Aidha Waziri Kagasheki alisema kuwa atavifuta vibali ambavyo
havikutolewa
kihalali ili vigawiwe upya.
Uvamizi
Waziri Kagasheki
alipata fursa ya kutembelea Kijiji cha Kibengu kujionea hali ya uvamizi
wa
misitu ulivyo. Katika kijiji hicho baadhi ya watu katika kitongoji cha
Mgwao walivamia
msitu wakajenga makazi na sasa wameshi ndani
ya hifadhi kwa muda wa miaka 30.
Waziri Kagasheki
alisema kuwa mwaka jana kamati mbili ziliundwa, moja ya Wizara na
nyingine ya
Kitaifa, ili kuchunguza migogoro ya mipaka ya hifadhi nchini. Taarifa za
kamati
hizo ambazo zilifika Saohill sasa zinachunguzwa ili mapendekezo yake
yachangie
katika kutoa uamuzi kuhusu uvamizi katika Shamba la Saohill na sehemu
zingine
za hifadhi nchini.
Awali, akisoma
taarifa ya Wilaya ya Mufindi kwa Waziri, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi
Evarista Kalalu
alisema kuwa wanachi wa vijiji sita vikiwemo Ihomasa na Udumuka
vimevamia eneo la misitu ya asili
iliyoko Sao Hill, kama vile Mufindi Scarp, na kufanya shughuli za kilimo
kwa
kati ya miaka 10 hadi 40.
Vile vile, Mkuu
wa Wilaya ya Mufindi alisema kuwa eneo la zaidi ya Hekta 1,000
linalomilikiwa
na Samba la miti Saohill limevamiwa na watu
wanaotokea vijiji vya Wamimbwale, Usokami, Kibengu, Igeleke, Mapanda na
Kitasengwa vyote vya Wilaya ya Mufindi kwa muda wa kati ya miaka 25 hadi
30.
[MWISHO]
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA
MALIASILI NA UTALII
Simu:
+255 784 468047


