MATOKEO YA DASARA LA SABA MKOA WA IRINGA NA NJOMBE ,HAWA NDIO WANAFUNZI 10 BORA


Afisa  elimu mkoa  wa Iringa Joseph Mwinyikambi akisoma majina ya  wanafunzi kumi bora
Katibu  tawala wa mkoa wa Njombe Mgeni Buriani akihitimisha kikao hicho
Mbunge  wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akichangia katika kikao  hicho leo mjini Njombe

Na Francis Godwin
Afisa  elimu mkoa  wa Iringa Joseph Mwinyikambi  leo amewataja   wanafunzi kumi bora kwa upande wa  wasichana na  wavulana  waliofanya mtihani  wa darasa la saba mwaka huu  mkoani Iringa.

Wanafunzi kumi bora  kwa upande  wasichana  ni  Rosemary  Mchang’a kutoka  shule ya  Brookebond Mufindi ambae anakwenda  shule  ya  Kilakala, Alen Fabian Fundi kutoka St Dominic Savio Manispaa ya Iringa anayekwenda Kilakala , Josephine Kadodo kutoka  shule ya Bwawani Njombe anaekwenda Kilakala, Miriam Ambokile kutoka shule ya msingi Ukombozi Manispaa ya Iringa atakwenda  Kilakala, Rachel Msungu kutoka  Sipto Manispaa ya Iringa kwenda  Msalato  na Fausta Malema  kutoka Makungu Mufindi  kwenda Kilakala.

Wengine ni Jestina sanga kutoka St Charles   manispaa ya Iringa kwenda  Mtwara ufundi, Hadija Chivugo kutoka  wilolesi Manispaa ya Iringa kwenda  Lugalo, Leilah Mng’agi  kutoka mapinduzi manispaa ya Iringa kwenda  Kleruu na Oliver Laurent  kutoka kanani Njombe kwenda  Kilakala.

Kwa upande  wa  wavulana ni  David  Juma kutoka  kanani Njombe kwenda Ilboru , Evance  Kisanga  kutoka  Kibwabwa Iringa Mjini kwenda  Ilboru , Emmanuel Luvela kutoka  Kanani Njombe kwenda Mzumbe, Edward Ngilangwa kutoka kanani Njombe  kwenda Kibaha na Fransisco Ngoda  kutoka Lupalamwa ‘A” Iringa vijijini kwenda  Ilboru 

Wengine ni  Philemon Lwaho kutoka  Kibwabwa Manispaa ya Iringa kwenda  Mzumbe, na  Dickson Mdete  kutoka  St Dominic Savio  Iringa mjini kwenda Kibaha ,Alfris Abdalah  kutoka Southern Highlands Mufindi  kwenda  Ifunda ufundi  , Antony Komba kutoka Southern  Highlands  Mufindi  kwenda  Mzumbe pamoja na Onorati Nyakunga  kutoka Ihanganatwa Mufindi  kwenda Ilboru .


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo