Dodoma
Waandishi wahabari nchini wametakiwa kuisoma vizuri na kwa umakini katiba ili kuweza kuelewa na kuandika habari za katiba vizuri na kwa usahihi ili wasiweze kuipotosha jamii.
Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi mtendaji Tamwa kutoka kamati ya JUKATA Valerie Msoka wakati akitoa mada kwenye mafunzo ya kujenga uwezo kwa waandishi wa habari katika mchakato wa katiba mpya Tanzania iliofanyika mkoani Dodoma.
Alisema kuwa wako baadhi ya waandishi wa habari hawana tabia ya kuisoma katiba kinachohusu katiba hivyo wanapaswa kuisoma vizuri katiba nakuweza kuripoti vizuri habari za katiba mpya nasi kwenda kinyume cha hapo.
Alieleza kuwa klabu za waandishi wa habari zinatakiwa pia kutumika katika kuhamasisha wanajamii kwa ujumla kuchangia kikamilifu katika mchakato wa katika mpya.
Alisema kuwa vyombo vya habari ni sehemu ya jamii mara zote vimekuwa vikijitambulisha kama watetezi wa wananchi pia vimechangia sana kaika kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali.
Aliongeza kuwa waandishi wahabari watumiwe kikamilifu katika kusukuma na kuengeneza ajenda za wananchi katika mamlaka zinazohusika.
Kwa upande wake mwenyekiti wa jukwaa la katibaTanzania Deus Kibamba alisema kuwa kwa upande wa jamii ya wafugaji wamekuwa na juudi za kushiriki katika kuchangia kuhusu maoni ya katiba yao na wameweza kujiokeza kwa wingi .
Aliendelea kusema kuwa wafugaji hao wameanza vizuri tofauti kwa miaka mingine, wakati wakiwa wanacunga mifugo yao tume inatakiwa kwenda katika maeneo ya malisho ili kuweza kuwaelimisha wafugaji hao.
Alisema kuwa mikakati mikubwa inahitajika sana kwaajili ya kuhamasisha wafugaji ao kaika maeneo yao wanayofugia mifugo yao ili nao waweze kuchangia mchakato wa katiba mpya.