Na Fortunatha Ringo-Manyara
MKUU wa Mkoa wa Manyara Elastol Mbwilo amewataka wananchi Mkoani Manyara kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Sinai kwa ajili ya kumpokea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete .
Ombi hilo amelitoa wakati akiongea na Waaandishi wa Habari katika mjini Babat,Mkuu huyo alieleza kuwa katika ziara yake Rais Kikwete anatarajia kuwasili mjini Babati Nevemba 3 mwaka huu akitokea Mkoani Arusha ambapo majira sasa 6.30 mchana atafungua Barabara yenye kiwango cha lami kutoka Minjingu-Babati-Singinda sambamba na kuongea na wananchi.
Alisema kuwa saa 10.jioni Rais atazindua mradi wa maji na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya Babati hadi bonga kwa kiwango cha lami.
Aliongeza kuwa novemba 4 saa 2.00 asubuhi ataondoka Babati kuelekea Singida kupitia Katesh-Wilayani Hanang ambapo njiani ataongea na wananchi sambamba nakumuona mwananchi ambaye ni mbunifu wa zana za kilimo na kuona mradi wa Ngozi.
Aidha kufuatia hayo alibainisha kwa kuwa Rias anakuja kufanya matukio makubwa yanayofaa kwa wananchi wa Mkoa wa Manyara,kwani kwa muda mrefu wananchi walikuwa wakihangaika kwa kusafiri kwani walikuwa wakisafiri kwa muda wa masaa 4-5 kutoka Babati hadi arusha lakini hivi sasaa baada ya kukamilika kwa lami wananchi wamekuwa wakisafiri kwa muda wa lisaa limoja na nusu tu.
Amewataka wananchi vijiji na vitongoji vyake hata na vijiji vya mikoa ya jirani wanatakiwa kufika kwa wingi kumpokea rais kwani ni kati ya ahadi yake wakati wa uchaguzi ambapo watakapokija kwa wingi ndipo atakapopata moyo wa kuweza kuendelea kusaidia mkoa huo.
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na maji Taka (BAWASA) amefafanua kwamba Mradi utakaozinduliwa umedhaminiwa na program ya maendeleo ya maji ambao umegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 5.9/=
Aliendela kusema kuwa mradi huo utakuwa unauwezo wa kuhudumia watu 77,000 sawa na asilimia 83% tofauti na awali ambapo watu waliokuwa wakipata huduma hiyo ya maji walikuwa 53,00 sawa na aslimia 23 %.
Kwa upande wake meneja wa wakala wa Barabara Mkoa wa Manyara-TANROADS Yohani Kasaine alisema kwamba Barabara hiyo ya Minjingu-Singida ina urefu wa km223.5 na umegharimu kiasi cha shilingi bil 220 tu.
Pia barabara nyingine atakayozindua na kuweka jiwe la msingi ya kutoka Babati-Bonga –Mayamaya ina urefu wa kilometa 19 na itakagharimu kiasi cha shilingi bil.19