MVUA YALETA MAAFA NJOMBE

 Licha ya nyumba kuezuliwa na kuvunjwa kwa miti lakini maafa mengine ni ya miti kuangukia nyumba.
Miti nayo yavunjwavunjwa katika mitaa mbalimbali mjini Njombe hususani kibena.
Hadi majira ya saa sita mchana ya leo barafu ilikuwa imetandaa mitaani katika mitaa ya kibena,Kihesa,Mjimwema na maeneo ya NUNDU ambako nyumba 35 ziliezuliwa.

Hii ndio hali ilijitokeza baada ya kuanguka kwa mvua kubwa mjini Njombe.
Wakati mitaa ya kibena mjini Njombe ikikumbwa na maafa baada ya kutokea kwa mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali nako kijijini Nundu katika halmashauri ya mji huo maafa hayo yamezikumba nyumba 35 zikiwemo mbili za walimu.
MTANDAO HUU Umefika kijijini humo na kushuhudia nyumba zilizoezuliwa pamoja na kuteketeza mazao yalikuwa shambani pamoja na
chakula kilichokuwepo ndani ya nyumba hizo.

Wakizungumza baada ya maafa hayo baadhi ya wahanga wa kijiji hicho wamesema kuwa hadi hivi sasa wameshapata hasara ya mali mbalimbali ambazo thamani yake bado haijafahamika huku wakiiomba serikali kuwasaidia katika maafa hayo.
Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Nundu bwana Winfred Mbangala na Afisa mtendaji wa kijiji hicho bwana Donatus Mlowe wamesema kuwa hadi sasa wanaendelea na kufanya tathmini ya mali na nyumba zilizokumbwa na maafa hayo huku jitihada za kuwasaidia zikiendelea.

Afisa Mtendaji huyo amesema kuwa kati ya vitongoji vitano vya kijiji hicho viwili ndivyo vimekumbwa zaidi na maafa hayo na kufikisha idadi ya nyumba 35 zikiwemo mbili za walimu katika shule ya msingi Nundu.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Njombe bwana George Mkindo
amesema kuwa kwa taarifa za awali zinaeleza kuwa halmashauri yake hadi sasa ni zaidi ya nyumba 100 zilizokumbwa na maafa hayo ukiwemo mtaa wa kihesa ambako takribani nyumba 60,zimekumbwa,nyumba 9 katika kata ya Mjimwema na maeneo ya Hagafilo ambako nyumba mbili zimeezuliwa.
Hata hivyo Bwana Mkindo
amesema kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa baadhi ya nyumba zimekuwa zikijengwa kwa kiwango cha chini bila kuzingatia utaalamu wa kiujenzi ikiwa ni pamoja na kutofunga koa kwenye paa kwa ajili ya kushikilia mabati na mbao.

Sanjali na hilo lakini pia amewataka wananchi hao kuongeza bidii ya upandaji miti kuzuia jangwa ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwasaidia wale waliokumbwa na maafa hayo kwa kuwapa hifadhi wakati ukarabati ukiendelea.
 

Ameongeza kuwa kutokana na maafa hayo halmashauri hiyo kwa sasa inaangalia jinsi ya kuwa na mfuko wa maafa huku wakiwa tayari wamefanya mawasiliano na mkuu wa wilaya ya Njombe anayehusika zaidi na suala la maafa 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo