Picha hizi zinaonesha jinsi moto ulivyounguza miti katika baadhi ya mashamba katika kijiji cha Ludihani wilayani Makete
Kwa mujibu wa taarifa alizozipata mwandishi wa mtandao huu, kutoka kwa afisa mtendaji wa kijiji hicho Dakta Mahenge ni kwamba umesababishwa na wakulima wanaoandaa mashamba yao katika kijiji hicho kwa ajili ya kilimo
Lakini pia amesema watu wengi hawana desturi ya kujitokeza kuzima moto pindi wanapoitwa kusaidia kuuzima
Kama kijiji, wametoa amri kuwa ni marufuku mtu kuanzisha moto kwenye mashamba bila kibali kutoka kwenye ofisi yake