Ufafanuzi huo umefuatia Vipeperushi vinavyodaiwa kusambazwa mjini Dodoma kwamba BASHE na kundi lake limepanga kuwashawishi wajumbe wa mkutano mkuu kupiga kura za maruhani ili Rais KIKWETE asiwe na uongozi wa kofia mbili ikiwemo ile ya Uenyekiti wa Taifa wa CCM.
Akifafanua BASHE amesema, kwa mfumo wa kiuongozi ndani ya CCM ni mwendawazimu pekee anayewaza kwamba suala hilo linawezekana na kwamba kauli ya iliyotolewa na mmoja wa kada wa chama hicho AGUSTINO MATEFU juu ya kumpunguzia kura rais ni mkakati uliopangwa ili kumdhalilisha Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Ili kuondoa utata wa juu ya anayehusika kuwatuma vijana wanaoeneza chuki na makundi ndani ya CCM, Bashe hapa anamtaja mmoja wa Mawaziri wa awamu ya ndani kwamba anaendesha mchezo mchafu ili kujisafishia njia ya Urais mwaka 2015.
Wakati hayo yakitokea tayari maandalizi ya shughuli za ufunguzi wa mkutano mkuu zimekamilika na wajumbe wamekwishawasili mjini tayari kuwachagua viongozi mbalimbali katika Ukumbi wa mikutano Kizota uliopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Chanzo: millardayo.com