Wazazi na walezi wametakiwa kushiriki vikao vya maendeleo ya elimu ikiwemo kujenga mahusiano na ushirikiano mzuri na walimu katika kufuatilia taaluma ya wanafunzi.
Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi wa shule ya awali na msingi ya mchepuo ya lugha ya kingereza ya Deira iliyopo Wilayani Babati Mkoani Manyara Nada Shauri katika kikao cha wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo mkoani manyara.
Alieleza kuwa wazazi,walezi wamekuwa wakitumia muda mwingi kufanya shughuli za mitaani na kusahau maendeleo ya elimu ya watoto wao hali ambayo imekuwa ikichangia kushuka kwa taaluma za wanafunzi wao na kuishia kuwatupia lawama walimu.
“Kwakweli sisi wazazi na walezi tumekuwa na tabia ya kufanya shughuli na kusahau kufuatilia maendeleo ya watoto wetu lakini mwisho wa siku mnawatupia lawama walimu kwamba hawafundishi vizuri”Alisisitiza Shauri.
Aidhi alisema kuwa wazazi wanapaswa kuwajibikana kutowaruhusu watoto wao muda mwingi kutumia kucheza na kufanya shughuli za nyumbani kwani itasaidia kuongeza kasi ya kufanya vizuri katika mitihani yao ya kumaliza elimu msingi.
Aliendelea kusema kuwa wazazi na walezi wanapaswa kutotegemea elimu pekee anayopata mwanafuzni awapo shuleni pia wanatakiwa kuwanunulia watoto wao vitabu mbalimbali vya kujiongezea maarifa kwani si kila somo analipata shuleni.
Vilevile wazazi na walezi wanatakiwa kushirikiana kwa karibu pamoja na walimu katika kutafuta mbinu mbadala ambazo zinapelekea mwanafuzni kufaulu mitihani ya majaribio na hata ile ya kumaliza elimu kufanya hivyo ni kuweza kufanikisha taaluma.
Nao wao wazazi wa wanafunzi hao,walibainisha kuwa kwa kuwa walimu ndio wanaochukua muda mwingi kukaa na wanafunzi wao wanapaswa kuwasiliana na wazazi pale kwenye mamatizo yanayohusu wanafunzi badala ya kutoa lawama kwa wazazi ambao wamekiri maranyingi hawana muda wa kufuatilia maendeleo ya watoto wao.
Pia wazazi na walezi hao wametoa pongezi kwa uongozi wa shule hiyo kuwa na utaratibu wa kuitisha vikao vya wazazi kwa ajili ya kujadili namna ya kuboresha taaluma na kukabiliana na changamoto katika sekata ya elimu,hivyo walidai watashirikiana na walimu kwa lolote litakalosaidia kuongeza taaluma shuleni hapo.