Meya wa Jiji la Dar Es Salaam Isaya Mwita aongoza Madiwani Kufanya Ukaguzi

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu NyerereJoseph Butiku,akimkaribisha Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita na madiwani wa Jiji hilo walipotembelea kukagua ujenzi wa jengo la taasisi ya Mwalimu Nyerere liitwalo The Mwalimu Nyerere Foundation Square lililopo karibu na Bandari jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Elisa Shunda.

 Mzee Butiku akimuongoza Meya wa Jiji,Isaya Mwita kuingia katika jengo hilo pamoja na madiwani wa jiji la dar es salaam kwa ajili ya kwenda kukagua ujenzi wa jengo hilo

 Mkutano ukiendelea

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu NyerereJoseph Butiku akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo kwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita na madiwani wa jiji hilo aliongozana nao katik ukaguzi wa jengo hilo.

 Meneja Mradi wa Kampuni ya CRJE ya Afrika Mashariki,Thomas Lee inayojenga jengo hilo akitoa maelezo kwa madiwani sehemu za nyumba za jengo hilo na muonekano wake pindi ujenzi ukikamilika.

 Meneja Mradi wa Kampuni ya CRJE ya Afrika Mashariki,Thomas Lee inayojenga jengo hilo akitoa maelezo kwa madiwani sehemu za nyumba za jengo hilo na muonekano wake pindi ujenzi ukikamilika.

 Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akizungumza katika mkutano huo na uongozi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere na uongozi wa Kampuni ya Ujenzi wa CRJE Estate L.T.D kabla ya kukagua maendeleo ya jengo hilo jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Meya wa Manispaa ya Temeke,Abdallah Chaulembo,Diwani wa Kata ya Mwananyamala,Songoro Mnyonge na Diwani wa Viti Maalumu eneo la Mabibo,Leyla Hussein.

 Diwani wa Kata ya Mwananyamala,Songoro Mnyonge akizungumza kwa niaba ya madiwani wenzake katika mkutano na uongozi wa Kampuni ya Ujenzi wa CRJE Estate L.T.D kabla ya kukagua maendeleo ya jengo hilo jijini Dar es Salaam leo. Kulia Diwani wa Viti Maalumu eneo la Mabibo,Leyla Hussein.

 Ukaguzi ukianza katika jengo hilo

  Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere,Joseph Butiku (kushoto) wakiangalia mandhari ya jiji la sehemu na uzuri wa jengo hilo lililopokuwa ambapo wageni na watu mbalimbali watakaotembelea katika jengo hilo watapata faida ya kuona kwa urahisi uzuri na mandhari ya jiji la Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu NyerereJoseph Butiku (katikati) akizungumza jambo na Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita (kulia) wakati wa matembezi ya kukagua jengo hilo la taasisi ya Mwalimu Nyerere liitwalo The Mwalimu Nyerere Foundation Square lililopo karibu na Bandari jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Meya wa Halmashauri ya Kinondoni,Benjamin Sitta na Meya wa Temeke,Abdallah Chaulembo (wa kwanza kushoto) na Diwani wa Kata ya Kibondemaji,Abdallah Mtinika (CCM).

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu NyerereJoseph Butiku (katikati) akizungumza jambo na Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita (kulia) wakati wa matembezi ya kukagua jengo hilo la taasisi ya Mwalimu Nyerere liitwalo The Mwalimu Nyerere Foundation Square lililopo karibu na Bandari jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Meya wa Halmashauri ya Kinondoni,Benjamin Sitta 

 Picha ya pamoja baada ya ukaguzi

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu NyerereJoseph Butiku (katikati) akizungumza jambo na Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita (kulia) wakati wa matembezi ya kukagua jengo hilo la taasisi ya Mwalimu Nyerere liitwalo The Mwalimu Nyerere Foundation Square lililopo karibu na Bandari jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Meya wa Halmashauri ya Kinondoni,Benjamin Sitta na Meya wa Temeke,Abdallah Chaulembo (wa kwanza kushoto) na Diwani wa Kata ya Kibondemaji,Abdallah Mtinika (CCM). 

Muonekano wa jengo la The Mwalimu Nyerere Foundation In Dar es Salaam litakapokamilika lililopo karibu na Bandari jijini hapa.
Imeandaliwa na Elisa Shunda

JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo