RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajia kuwa na ziara ya
Kikazi Mkoani Kilimanjaro kuanzia Oktoba 28 -30 Mwaka huu ambapo
atazindua Miradi mbalimbali ya Kimaendeleo.
Akiwa Mkoani Kilimanjaro,rais Kikwete atazindua nyumba nane za wahanga wa mafuriko yaliyotokea katika kata ya Ndungu Mamba Miamba mwaka2009 pamoja na kuzindua kiwanda cha Tangawizi.
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Mkoa iliyotolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro bw.Leonidas Gama,alisema Rais Kikwete pamoja na kuzindua
kiwanda na nyumba hizo,pia atazindua shule ya sekondari wasichana ya
Asha Rose Migiro iliyopo wilayani Mwanga.
Pia rais Kikwete atazindua barabara ya Rombo maarufu kama barabara yaAfrika ya Mashariki pamoja na barabara ya kwenda Masama.
Aidha gama alisema pamoja na kuzindua miradi hiyo,pia rais Kiwete
katika ziara yake hiyo atazungumza na wananchi wa Manispaa ya Moshi na baadae kuendelea na majukumu mengine.
Kuhusu Miradi iliyopo wilayani Moshi Vijijini na Siha,Gama alisema
atakuja awamu nyingine na kuwataka wananchi wa maeneo husika
kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumlaki sambamba na wale wa moshi
vijijini walio karibu na manispaa kufika ili kumsikiliza rais
atakachosema.
Katika ziara hiyo ya rais kikwete ya kuzindua nyumba nane za wahanga
wa mafuriko,yaliyotokea usiku wa kuamkia Novemba 11 mwaka
2009,familiya zipatazo 33 ziliathirika na nyumba saba zilisombwa na
kufunikwa na maporomoko ambapo watu 24 waliopoteza maisha ambapo maafa hayo yalivikumba vijiji viwili ambavyo ni kijiji cha goha na kijiji
cha kambeni ambacho hakuna aliyeripotiwa kupoteza maisha.