WANAFUNZI 60 WASHINDWA KUMALIZA ELIMU YA SEKONDARI SHULE YA QASH MKOANI MANYARA


Imeelezwa kuwa zaidi ya Wanafunzi wapatao 60  wameshindwa kumaliza elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Qash iliyopo wilayani Babati Mkoani Manyara.

Haya yameelezwa na  mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne  Rozina Dabil wakati akisoma risala kwenye  mahafali ya tatu ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Qash yaliyofanyika shuleni hapo  Manyara.

Alieleza kuwa  kuwa kati ya wananfuzni 163 waliokuwa wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2009 waliofanikiwa kuhitimu ni 103 walioshindwa kumaliza ni 60 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mimba,utoro.

Alisema kuwa  pamoja na changamoto hiyo pia shule hiyo inakabiliwa na tatizo la upungufu wa walimu jambo ambalo huwafanya wananfuzni kupata matokeo mabaya katika mitihani na majaribio.

Aliongeza kuwa  shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya maji hali inayosababisha wanafuzni kuchelewa vipindi vya darasani kwenda kutafuta maji kwa matumizi ya Chakula.

Alitoa mapendekezo kwa mgeni rasmi kuwa shule isaidiwe mahitaji yote ikiwemo vitabu vya kutosha,walimu,maabara ya kisasa,bwalo la kulia chakula,umeme,vifaa vya kufundishia,maji safi na salama yanapatikana kwa uhakika.

Pia alitaja mafanikio yaliyopatikana katika shule hiyo kuwa ongezeko la wanafunzi wanaojiunga  na kidato cha kwanza,kuboresha mazingira,kupanda miti ya kivuli na miti ya matunda,kutengeneza viunga vya maua.

Naye Mkuu wa Shule hiyo  Abubakary Kiritto alibainisha kuwa  shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali likiwemo la shule kuwadai wazazi na walezi zaidi ya shilingi milioni 12 kwa kutolipa michango hali inayopelekea uendeshaji wa shule kuwa mgumu.

Aidha aliendelea kusema  kuwa ingawa shule hiyo ilianzishwa mwaka 2007 lakini hadi sasa haina hata nyumba moja ya walimu hali inayosababisha walimu kupanga nyumba katika mji mdogo wa gallapo umbali wa zaidi ya km5.

Pia kutokana na  changamoto hizo mkuu wa shule hiyo ameiomba  Serikali kutoa msaada wa hali na mali ili kuweza kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo ili kuweza kuweka mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo