Wito umetolewa kwa wananchi wa Tarafa ya Bassotu Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara wametakiwa wasiendeshe shughuli za kilimo na ufugaji pembezoni mwa ziwa Bassotu kwani husababisha kina chake kupungua hivyo kuliathiri eneo hilo.
Wito huo umetolewa na Mratibu wa asasi ya Cedesota,Jackson Muro kwenye mdahalo wa mabadiliko ya tabia nchi na namna ya kupunguza athari zake ulioandaliwa na Mtandao wa asasi za kijamii mkoani Manyara (Macsnet) na The Foundation for Civil Society na kufanyika Bassotu wilayani Hanang’ mkoani Manyara.
Alisema kuwa udongo huo mlaini unapoingia katika ziwa Bassotu hutengeneza tabaka lenye huziba vishimo vidogo vidogo vilivyopo chini ya ziwa hilo ambavyo vinavyonya maji na kuyatitirisha ziwani.
Aidha aliwataka wananchi wanaolizunguka ziwa hilo kutoendesha shughuli za kibinadamu pembezoni mwa ziwa hilo ili kutoendeleza athari hizo na kutosingizia kuwa ni matatizo yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchini.
Kwa upande wake Ofisa Ardhi na Maliasili wa halmashauri ya wilaya ya Hanang’ Kianga Mdundo alieleza kuwa sheria ndogo ya ziwa Bassotu inawataka wakazi wa eneo hilo kutofanya shughuli za kibinadamu nje ya mita 200 ya ziwa hilo.
Alisema kuwa sheria hii mlijiamulia wenyewe na watekelezaji wa kwanza wa sheria hiyo mnatakiwa muwe ninyi wenyewe siyo Mkurugenzi wa wilaya kwani watu wa Bassotu ndiyo mpo ziwani hivyo mtunze mazingira yenu.
Naye Diwani wa kata ya Bassotu,Samwel Qawoga amewaasa wananchi wa vijiji vya Bassotu na Mulbadaw ambao wananufaika na ziwa hilo kuchukua changamoto zilizopo ili kuhakikisha wanalitunza vema ziwa hilo.
Aliendelea kusema kuwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kuwa ni suala la kitaifa na kimataifa,wakazi wa eneo hilo wanapaswa kusimama kidete katika kuhakikisha kwamba wanayatunza mazingira yanayowazunguka.