SERIKALI Wilayani Rorya mkoani Mara imeonya
kuwa
haitasita kuwachukua hatua kali kwa watendaji katika halmashauri hiyo
watakaoshindwa kusimamia kikamilifu mapato ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha
fedha za miradi zinazotolewa inatekelezwa kwa wakati na kwa miradi
ambayo
imekusudiwa.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya
Rorya Bw
Elias Goroi,katika kikao la kawaida cha baraza la madiwani amasema
mapato ya
halmashauri hiyo yanapaswa kuongezeka ili kuwa na uwezo wa
kuhudumia miradi ya wananchi.
Amesema inasikitisha kuona kila mwaka
halmashauri hiyo inakubwa na dosari kubwa katika ukaguzi wa hesabu zake
hivyo
serikali sasa haitakuwa na huruma kwa wakuu wa idara watakaobainika
kuhusika
katika matumizi mabaya ya fedha za umma.
Ameongeza kuwa Halmashauri hiyo inapaswa
kuhakikisha fedha zinazotolewa zinatumika vizuri na kwamba nidahamu
itumike katika ukusanyanji wa mapato katika vyanzo vyote vya vya wilaya
hiyo na
kamwe wasisite kuwachukulia hatua wazabuni watakashindwa kwenda na kasi
hiyo.
Halmshauri ya Rorya kwa kipindi cha Julai
2011 hadi -
Juni 2012 kupitia vyanzo vyake imekusanya kiasi cha shlingi zaidi
milioni 595.2 ikilinganishwa na makisio ya kukusanya kukusanya kiasi
cha zaidi ya shilingi bilioni 1.5 kwa kipindi hicho.