SERIKALI
wilayani
Bunda mkoani Mara,imewaagiza viongozi wenyeviti na watendaji wa vijiji
vyote vya wilaya hiyo, kuandaa mipango maalum ya kilimo kwa kuanda
madaftari ya
kuorodhesha mashamba ya kila kaya katika kuhakikisha wilaya hiyo sasa
inaondokana na tazizo la njaa linalojitokeza mara kwa mara.
Mkuu
wa wilaya
ya Bunda Bw Joshua Mirumbe,amesema tayari viongozi hao wa
vijiji,wameagizwa
kuandaa madaftari hayo ambayo yatatumika kuorodhesha mashamba ya mazao
ya
chakula na biashara kwa kila kaya kuanzia sasa.
Kwa
sababu hiyo
mkuu huyo wa wilaya ya Bunda,amesema Serikali kamwe haitasita
kuwakamata
na kuwafungulia mashitaka viongozi hao wa vijiji watakashindwa
kutekeleza agizo
hilo na kuweka mipango mizuri ya kufanikisha kilimo ambacho pia
kinalenga
kuinua uchumi wa wananchi.
Hata
hivyo mkuu
huyo wa wilaya ya Bunda, amesema serikali wilayani humo imeanzisha
utaratibu wa
kupima utendaji wa kila kiongozi wa kijiji kwa jinsi anavyojishughulisha
na
utatuzi wa kero zinazowakabili wananchi katika eneo lake pamoja na
kutanguliza mbele utawala wa bora unazingatia sheria na kwamba
atakaeshindwa kufanya hivyo ni vyema akajiondoa mwenyewe katika nafasi
hiyo.
