Wananchi
wa Nyamongo Wilayani
Tarime Mkoani Mara wamelaani kitendo cha
polisi kupiga kwa mabomu na risasi za moto wananchi
maarufu kama intruda katika
mgodi wa North Mara Barrick na
kwamba hawapaswi kufanya mauwaji kwakuwa nao ni miongoni kati ya polisi
wanaojihusisha na uintruda.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti
na gazeti hili walisema kuwa mbali na wananchi kudaiwa kuvamia
mgodi wapo pia polisi ambao uiba mawe
ya dhahabu ndani ya mgodi huo kisha kuuza mawe ya dhahabu
kwa wananchi na kupatiwa fedha.
Chacha
Mwita mkazi wa
Nyangoto alisema kuwa kitendo cha
wananchi kuingia mgodini ni baada ya kupatiwa taarifa na askari polisi
wanaolinda mgodi mara tu dhahabu inapoonekana ambapo wananchi uwapatia
pesa
nakuwaruhusu kuingia mgodini ambapo hata hivyo wananchi hao uungana na
baadhi
ya polisi kuingia ndani ya mashimo ya dhahabu na kuchukuwa mawe yenye
dhahabu.
“Nashangaa
polisi wanawauwa
wananchi nawakati wao ndiyo chanzo
polisi ndiyo wanaosuka mipango yaani mchongo wanawaomba pesa
wananchi
kisha wanaingia kwenye mashimo wakiona
hali ya usalama ni mbaya au gari la mzungu linapita wanapiga watu mabomu
na
risasi kuonyesha kuwa wananchi wamevamia mgodi polisi ndiyo wanalinda
mgodi na
ndiyo wanaojua kuwa mahali Fulani wamemwaga mawe ya dhahabu”alisema
Mwita.
Mwananchi
mwingine ambaye
hakutaka jina lake
litajewe alisema chanzo
cha uvamizi wa mgodi kinatokana na mitandao ya polisi ndani ya mgodi
ambao wapo
kwa ajili yakulinda lakini lengo lao ni
kuchukuwa mawe yenye dhahabu nakuyaunza kwa wananchi.
“Polisi
wanaiba dhahabu hivi
karibuni kuna polisi walichukuwa mawe ya
dhahabu wakawauzia wananchi wakapata mamilioni ya fedha tunajua na
tunawafahamu
kwasababu mawe ya dhahabu yanauziwa hapahapa Nyamongo tena pesa hizo
wanazitumia kwa starehe wanaita funga baa wananunua creti za bia
wanafanya
mashindano ya kunywa bia,wakiwabaini wananchi wana mawe ya dhahabu
wanawanyang’anya kisha wanawatafuta wateja wao na kuwauzia ni kutu cha
wazi na
kinafahamika hakuna asiyejua’alisema,
Hata
hivyo
vyanzo vya habari vingine vina sema kuwa
mauwaji ya watu wawili yaliyotokea wiki iliyopita katika mgodi wa
Nyamongo
inadaiwa kuwa ilikuwa ni plani ya polisi ambao baadhi yao namba zao za
simu tunazo akiwemo askari aliyedaiwa
kujeruhiwa na intruda siku ya mauwajiya wananchi ambapo RPC Justus Kamugisha
alisema kuwa askari mmoja No. E 6059 D/CPL Julius alijeruhiwa
na maintuda kwa kukatwa panga usoni na kupata majeraha mdomoni na
mgongoni.
Ambapo
kwa
maelezo ya vyanzo vya habari wanasema siku ya mauwaji askari huyo Julias
akiwa
na askari aliyefahamikwa kwa jina moja
Kimaro wa Musoma ambaye yuko rikizo kwa
matibabu lakini yuko Nyamongo akijihusisha na uintruda waliingia ndani
ya shimo
la dhahabu maarufu kama piti
Polisi
hao wanadaiwa kuwa walichukuwa mawe ya dhahabu ambapoa hata hivyo
kutokana na intruda kuwa wengi walipata
hofu na hivyo kuwatawanya kwa mabomu na risasi na hivyo kusababisha vifo
vya
watu 2 na majeruhi mmoja ambapo pia wananchi nao waliweweza kumjeruhi
kwa mawe askari Julias.
Hata
hivyo
Kamanda wa polisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha alipohojiwa kujua kama
anataarifa ya madai ya polisi wake
kujiusisha na wizi wa mawe ya dhahabu mgodini hapo licha ya kuwa ni
walinzi wa
mgodi hakuwa tayali kusema chochote
badala yake alimtaka mwandishi amsaidie kufanya uchunguzi ambapo
pia
alisema hataki kuona mwandishi wa habari ofisini kwake kwa madai kuwa
wanatoa
tarifa za uongo.
