POLISI MKOANI MARA LAWAMANI TENA

 
WANANCHI wa mji wa Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara,wamelaani kitendo cha askari wa jeshi la polisi kutumia nguvu kubwa kwa kuwapiga mabomu na risasi za moto wananchi wanaokota mawe katika mgodi  wa ABG  North Mara jambo linalosababisha mauaji na vilema vya kudumu kwa wananchi.
 
Wamesema kuwa polisi hawapaswi kufanya vitendo hivyo vya mauji ya wananchi kwakuwa baadhi yao ni miongoni mwa watu wanahusika na vitendo hivyo vya wizi huo wa mawe katika mgodi huo.
 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti,wanasema ni kweli wananchi wamekuwa wakiingia katika maeneo ya mgodi huo kwaajili ya kuokota mabaki yam awe lakini pia polisi wanakuwa zamu wamekuwa wakibariki vitendo hivyo kwa kupewa fedha na wananchi.
 
Wamedai kuwa mbali na polisi hao kupewa fedha na kuruhusu wananchi kuingia ndani ya mgodi kabla ya kutofautiana na kuanza kuwashambulia kwa mabomu pia wamekuwa wamekuwa wakiiba mawe ya dhahabu ndani ya mgodi kisha kuyuza kwa wananchi.
 
Mmmoja ya wananchi hao Bw Chacha Mwita mkazi wa Nyangoto,amesema kuwa  kitendo cha wananchi kuingia mgodini ni baada ya kupatiwa taarifa na askari polisi wanaolinda mgodi mara tu dhahabu inapoonekana ambapo wananchi uwapatia pesa nakuwaruhusu kuingia mgodini.
 
Kamanda wa polisi mkoa kanda maalum ya Tarime na Rorya ACP JUSTUS KAMUGISHA,amekiri kupata taarifa hizo lakini amesema hakuna mwananchi anajitokeza hadharani kuwataja polisi hao ili hatua kali za kinidhamu na kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo