
Timu ya wanahabari wa mkoani Mbeya kupitia Chama cha Wanadishi
wa Habari Mkoa wa Mbeya wakiwa safarini kuelekea Kijiji cha Busoka
Tukuyu wilayani Rungwe mkoani humo Ambapo Mwili wa marehemu Daud
Mwangosi aliyekuwa Mwakilishi wa Channel Ten anataraji kuzikwa baada ya
kupoteza maisha kwa kushambuliwa na bomu wakati wa fujo baina ya Polisi
na Wafuasio wa Chadema Iringa.

Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu, wa kwanza kushoto ndugu Joseph
Mwaisango akiwa ndani ya Basina waandishi wengine kuelekea katika Msiba
na Mazishi muda huu.

Safari inaendelea

Hapa Mambo yanaenda na safari inaendelea kama kawaida , ni
asubuhi kabisa lakini tunajitahidi kuwaletea tukio zima Live moja kwa
moja.
Safari inaendelea

Hakika hakuna
Mwandishi wa habari hata mmoja aliye na Furaha wengi wanaonekana wakiwa
na uchungu, juu ya kifo cha Mwandishi mwenzao. SOURCE:Mbeya Yetu Blog