Baadhi ya washiriki
Bi Imelda Urio kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC akitoa mafunzo
Bw. Ngajilo, mmoja wa wasaidizi wa kisheria
wasaidizi wa kisheria wakijadili jambo nje ya ukumbi
Wasaidizi wa kisheria kutoka
kwenye kata zilizopo wilayani Makete, wanapatiwa mafunzo ya sheria mbalimbali
na kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) kwa lengo la kuzidi kutoa msaada
wa kisheria kwa wananchi wa maeneo hayo
Mafunzo hayo ya siku tatu yamefanyika
wilayani hapo kwa kuwakutanisha wasaidizi wote wa kisheria waliopo wilayani
hapo kwa lengo la kuzidi kuwajengea uwezo wa kisheria
Mkufunzi kutoka kituo cha sheria
na haki za binadamu Imelda Urio amewataka wasaidizi hao wa kisheria kuzingatia
sheria wanazofundishwa na pia wawe mdsaada mkubwa wa wananchi wanaohitaji
msaada wa kisheria
Miongoni mwa sheria
walizofundishwa wasaidizi hao hadi hii leo ni pamoja na sheria ya ndoa, sheria
ya ajira na mahusiano kazini pamoja na sheria ya ardhi
Wakizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo, wasaidizi hao wamesema kwa kiasi
kikubwa wanapiga hatua na kupata uelewa mkubwa zaidi wa kisheria ambao nao
wanautumia kuwapatia msaada wa kisheria wananchi wa maeneo yao
“Unajua watanzania wengi
hatufahamu sheria na ndio maana matatizo ya kisheria yanapotukumba tunakuwa
hatuna la kufanya, mafunzo haya yanatupa mwanga walau wa kujua wapi pa kuanzia
hili ni jambo jema sana, na tunaomba kituo cha sheria na haki za binadamu
kiendelee kutoa mafunzo haya hata maeneo mengine hapa nchini”alisema msaidizi
wa kisheria Nebart Sigala kutoka kata ya Lupila wilayani Makete
Mafunzo hayo yaliyoanza jana
yanatarajiwa kuhitimishwa hapo kesho



