MAHAKAMA ya Hakimu
mkazi mkoa wa
Mara Imetoa hukumu ya
kesi ya jinai namba 360 ya mwaka
2010 iiliyokuwa ikiwahusu watuhumiwa sita.
Watuhumiwa hao sita
wanadaiwa
kumteka na kumshambulia vibaya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha
Wananchi CUF
wilaya ya Musoma mkoani Mara Bw Didi Musira Koko.
Katika tukio hilo
la kushambuliwa
kwa Bw Didi Musira Koko aliyekuwa Mwenyeki wa CUF Manispaa ya Musoma
mkoani
Mara ilisababisha kuumia mguu ambapo kwa
mujibu wa taarifa za kitabibu ilionekana kuwa mfupa umehama lakini
haukuvunjika.
Watuhumiwa katika
kesi hiyo walikuwa ni Bw
Mapinguzi Muhere,Magori Zembwera na Geofrey
Marwa.Wengine ni Justine
Dida ,Dickson Anthony na Manumbu Magacha ambapo Mahakama iliwaachia huru
watu
watano waliokuwa katika kesi hiyo huku Bw Mapinduzi Mhere akikutwa na
hatia
Hukumu hiyo
iliyosomwa na Hakimu wa Mahakama
ya
Hakimu mkazi mkoa wa Mara Hussen Mushi
ilitoa adhabu kwa Bw Mapinduzi Mhere kifungo cha Mwaka mmoja Jela au
kulipa Faini
ya Shilingi laki Tatu
Tukio hilo
lililotokea Septemba 25
Mwaka 2010,lilitokea wakati Didi Musira koko akitoka katika mkutano wa
kampeni
wa aliyekuwa mgombea urais kupitia chama chama Mapinduzi CCM Rais Jakaya
Kikwete katika uwanja wa shule ya msingi Mukendo.
