JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro, linawashikilia wahamiaji haramu 10kutoka nchini Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini Kinyume cha sheria.
Mbali na wahamiaji hao jeshi hilo pia linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kuwasafirish wahamiaji hao katika eneo la kilema pofo na mjohoroni wilayani moshi mkoani hapa.
Akitoa taarifa
hizo za kukamatwa kwa wahamiaji hao pamoja na watu hao Kaimu kamanda wa
polisi mkoani Kilimanjaro Koka Moita, alisema kuwa septemba sita majira
ya saa tisa na nusu usiku katika eneo la Kilema pofo wilayani moshi
zilikamatwa pikipiki nne zilizo kuwa zimewapakia wahamiaji haramu
wapatao 8.
Alisema wahamiaji
hao haramua ambao wamebuni mbinu nyingine za kutumia usafiri aina ya
bodaboda walikamatwa wakiwa wametokea eneo la Taeakea wilayani Rombo
kueleka wilayani Hai ambapo walikuwa wamepanda pikipiki hizo kwa mtindo
wa mshikaki.
Akizungumzia tukio jingine kamanda
Moita alisema kuwa septemba sita majira ya saa tisa na nusu usiku huko
katika eneo la Mjohoroni walikamata pikipiki tatu zikiwa zimewabeba
wahamiaji wengine sita wakitokea wilayani Rombo kuelekea wilayani Hai.
Alisema kuwa
wakati askari wakijaribu kuwatia nguvuni watu hao wahamiaji haramu wane
walifanikiwa kutoroka na kufanikiwa kuwakamatwa wahamiaji wawili pamoja
na madereva wa bodaboda hizo.
Aidha kamanda huyo
alisema kuwa madereva wa bodadoda hizo zote waanashikiliwa na jeshi la
polisi kwa tuhuma za kuwasafirisha wahamaiaji haramu kinyume cha sheri
na kwamba watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.