WAHAMIAJI HARAMU 24 WAKAMATWA MOSHI


 
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia wahamiaji haramu 24
ambao walikuwa wakihifadhiwa katika nyumba ya mkazi mmoja jina
limehifadhiwa)katika kijiji cha Jipe wilayani Mwanga.

Akizungumza na wanahabari,kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa
Costantine Maganga amesemawahamiaji hao waliingia nchini agusti 30
mwaka huu na kuhifadhiwa nyumbani kwa bw.YasinMrutu.

Amesema Raia hao wametokea nchini Ethiopia  na kufika nchini kinyemela
kwa lengolakuelekea afrikaya kusini  kwa kupitia nchini Zambia  na
kuongeza kuwa juhudi za wananchi wa wilaya hiyo za kutoa taarifa kwa
jeshilapolisindizo zilizofanikisha kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu.

Aidha amewataka wananchi hao kuendelea kushirikiana na jeshi hilo
ilikusaidia na kufanikisha utendaji kazi wa jeshi hilo ambalo kwa
kiasi kikubwa limekuwa likifanya kazi kwa karibu kabisa na wanajamii..

Naye kaimu kamishna wa uhamiaji  wilayani mwanga na same Fustus Selele
amesema wimbi lawahamiaji haramu limezidi kuongezeka kutokanana
mtandao uliopo sanjari na watanzania kujiingiza kwenye biashara hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo