MWANAFUNZI AFA AKICHEZA KISIMANI


 
MWANAFUNZI wa shule ya msingi  Mkapa, Matayo John (9) iliyopo  wilayani Same mkoani kilimanjaro, amefariki dunia baada ya kushika mota
iliyokuwa  imewashwa kwa ajili ya kupandisha   maji ya kisima.

Kamanda  wa polisi mkoani hapa Robert Boaz,amethibitisha  kutokea kwa
tukio hilo na kwamba lilitokea august 29 mwaka huu majira ya 11:30 wilaya humo wakati mtoto huyo akicheza na wenzake.

Kamanda alisema mtoto huyo aligusa mita ya kupandishia maji ya kimasima  ambayo ilikuwa imewashwa na kufariki kwa kupigwa shoti ya umeme

Boaz alisema mota hiyo ilikuwa nyumbani kwa Rajabu Abdala ambapo marehemu  huyo alikuwa akicheza maeneo hayo akiwa na wanzake.

Kamanda amewataka wazazi na walezi kuangalia watoto wao wakati wanatumia vitu vinavyoweza kuhatarisha maisha yao ili kuweza kuepusha vifo visivyo vya lazima kwa watoto.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo