Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la
Tanzania Alhaj Adam Kimbisa (kushoto) akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) na kuviomba vyombo vyao viweze kutambulisha timu ya
wabunge hao tisa kwa watanzania ili wapate kuwafahamu kama wawakilishi
wao wanaosimamia masuala ya taifa. Kulia ni Mbunge Angela Kizigha ambaye
ni Mwenyekiti wa kamati ya biashara na uwekezaji na kamati ya mazingira
katika bunge hilo. Picha na Anna
Nkinda – Maelezo
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Angela Kiziga
(kulia) ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya biashara na uwekezaji na
kamati ya mazingira akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo
jijini Dar es Salaam kuhusu tofauti ya kiuchumi na maendeleo baina ya
nchi tano wanachama wa jumuia hiyo . Vikao vya Bunge hilo ambavyo ni vya
wiki mbili vinatajiwa kuanza kesho jijini Nairobi Nchini Kenya. Kushoto
ni Mwenyekiti wa Wabunge hao Alhaj Adam Kimbisa.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Twaha Issa Taslima
akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mkataba wa Jumuia ya
Afrika Mashariki ambao wataufanyia kazi katika kikao cha Bunge
kinachotarajia kuanza kesho mjini Nairobi Nchini Kenya. Wabunge hao
waliongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa Idara
ya Habari (Maelezo) uliopo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania
Shy-Rose Banji (kulia) akiongea jambo na Abdullah Mwinyi (kushoto)
ambaye ni Mjumbe wa kamati ya mahesabu ya fedha wa bunge hilo wakati wa
mkutano baina yao na waandishi wa habari uliofanyika leo katika ukumbi
wa mikutano wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam. Vikao vya
Bunge hilo ambavyo ni vya wiki mbili vinatajiwa kuanza kesho jijini
Nairobi Nchini Kenya
Mjumbe wa kamati ya mahesabu ya fedha wa bunge la Afrika
Mashariki Abdullah Mwinyi akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu
ujenzi wa uwanja wa Ndege unaoendelea huko Taveta nchini Kenya kwamba
hauna dhamira ya kuathiri uwanja wa ndege wa Kilimanjaro. Kulia ni
Katibu wa Wabunge hao Tawi la Tanzania Shy-Rose Banji .
Kutoka kusho ni Mjumbe wa
kamati ya mahesabu ya fedha wa bunge la Afrika Mashariki Abdullah
Mwinyi,Katibu wa Wabunge wa Afrika
Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Shy-Rose Banji, Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika
Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Alhaj Adam Kimbisa na Mbunge wa Bunge
la Afrika Mashariki (EALA) Twaha Issa Taslima
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Twaha Issa Taslima
akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo.
Katibu wa Wabunge wa Afrika
Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Shy-Rose Banji (kushoto) akiwaomba
waandishi wa habari waweze kutangaza umuhimu wa Bunge hilo na fursa
zilizopo kwa wajasiriamali hasa wanawake. Wabunge hao waliongea na
waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari
(Maelezo) uliopo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti, Alhaj Adam
Kimbisa na Mjumbe wa
Kamati ya Mahesabu ya Fedha wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdullah
Mwinyi.




