Sifa na salamu zinatolewa juu ya
waziri mkuu Meles Zenawi wa Ethiopia aliyeongoza kwa miaka mingi,
ambaye anazikwa katika mji mkuu, Addis Ababa.
Viongozi wa Afrka na kwengineko
wamekuwa wakionesha heshima zao pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda,
ambaye alisema Bwana Meles alitumia upeo wake mkubwa kuendeleza Afrika.
Maelfu ya wananchi wa Ethiopia - wengi wao
wakiwa wamevaa T-shirt nyeusi zenye picha ya Bwana Meles - wamejaa
kwenye medani kuu ya Addis Ababa.
Bwana Meles anasifiwa kuwa aliongoza maendeleo
ya Ethiopia, lakini piya alilaumiwa kwa kukiuka haki za kibinaadamu.
Aliyechukua nafasi yake, Hailemaruiam Desalegn,
ataongoza nchi hadi uchaguzi wa mwaka wa 2015.
SOURCE:BBC