Imebainika kuwa miradi mingi
inayoibuliwa na halmashauri/asasi mbalimbali na kuhitaji ufadhili wahisani mbalimbali inashindwa
kupatiwa ufadhili kutokana na wengi wao kuandika kuwa watatoa mafunzo kuliko
vitu vingine vya ziada ambayo vitatatua changamoto hizo
Kutokana na wengi kuandika kuwa
watatoa mafunzo kwa watu mbalimbali badala ya kuainisha njia nyingine za ziada
za kutatua changamoto zinazoikabili jamii, njia hiyo imeonekaka kuwakera
wahisani na kuona kuwa hakuna jipya litakalojitokeza katika changamoto hizo pindi
watakapotoa ufadhili
Akizungumza kwenye kikao cha
kuandaa mikakati ya namna wilaya ya Makete itatokomeza maambukizi ya virusi vya
UKIMWI kwa wananchi wake, Bi Alice kutoka shirika la umoja wa mataifa la
kuhudumia watoto ulimwenguni (UNICEF), amesema haikatazwi mipango hiyo kuwa na
kipengele cha kutoa mafunzo ili kukabiliana na changamoto husika, lakini
kinavyokuwa kikubwa inapelekea wafadhili kuwa na hofu ya kufanya nao kazi
“Wakati mwingine zile trainings
(mafunzo) zikiwa kubwa katika majadiliano wafadhili hawaipi kipaumbele kabisa
yaani wataifanya ya mwisho, na kama zipo fedha basi watafadhili, kwa sasa
tutazame zaidi njia nyingine za kufanya achilia mbali mafunzo” alisema bi Alice
Amsema umefika wakati kwa sasa
kuhakikisha kuwa waandikaji wa mikakati mbalimbali wahakikishe wanaainisha njia
mbadala ambazo zitamvutia mfadhili kuweza kufadhili zitakazotumika kutatua
changamoto zilizopo kwa jamii
