SUMA-LEE NA LINEX KWA PAMOJA WAACHIA NGOMA MPYA IITWAYO “BODA BODA!!”


MZINGO MPYA TOKA KWA PRODUCER MACHACHARI TOKA KULE PANDE ZA KIBAHA AITWAYE FUNDI SAMWELI CHINI YA STUDIO ZA USANII PRODUCTION. 
USHIRIKIANO WA UIMBAJI KATI YA SUMALEE PAMOJA NA LINEX  KATIKA WIMBO HUO HAKIKA NI WA KUVUTIA NA WENYE BASHASHA YA AINA YAKE…….BODA BODA NDIO JINA LA WIMBO HUO, AMBAO MAHUDHUI YAKE NI MAPENZI……..”MAPENZI YENYEWE NI YALE WA WATU WA HALI YA CHINI, YAANI YULE KIJANA WA KAWAIDA KABISA MWENDESHA BODA BODA AMBAYE AMECHUMBIA NA KUKATALIWA NA WAKWE  SABABU YA HALI YAKE YA MAISHA YA CHINI YA “DHOFU BIN HALI”  MWENDESHA BODA BODA…………..EBU SIKIA WIMBO HUU WENYE HISIA  YA AINA YAKE SAUTI MBILI TOFAUTI KATI YA LINEX (MJEDA)  NA YA SUMA LEE JINSI ZINAVYOLALAMIKA KWA HISIA UTADHANI WAO NDIO WAHUSIKA WA MKASA HUO………..WAMELALAMIKA KWELIKWELI..!! HUKU UPANGILIAJI WA VYOMBO NA MIDUNDO VIKIPANGWA KWA USTADI MKUBWA SANA NA MTU MZIMA FUNDI SAMWELI…………………..HAKIKA NI WIMBO WA KUVUTIA..!.
BY OWEN.
WIMBO       : BODA BODA
WASANII     : SUMA LEE & LINEX [KIGOTANG]
PRODUCER : FUNDI SAMWELI
STUDIO        : USANII PRODUCTION


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo