MKAZI mmoja wa kijiji cha Maneke katika kata
ya
Tegeruka wilaya ya Butiama, Bw Magwegwe Chiriso amelazwa katika hospital
ya
mkoa wa Mara baada ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi na
kisha
kumpora kiasi cha shilingi laki tisa.
Akizungumza katika wodi namba 8 ya
hosptali hiyo mjini Musoma majeruhi huyo amesema kuwa tukio hilo
limetokea juzi
majira ya saa 6 usiku baada ya watu hao kuvunja mlango wake kwa kutumia
jiwe kubwa maarufu kama Fatuma.
Amesema kuwa baada ya majambazi hao kubomoa
mlango huo
waliingia ndani majambazi wawili wakiwa na silaha za jadi ambapo
walimuamilisha yeye na mke wake wake wawape pesa kiasi cha shilingi laki
saba
huku wakiwakata kata kwa mapanga.
Amefafanua kuwa baada ya kuona wanazidi
kushambuliwa
zaidi aliwaonyesha fedha hizo zikiwa sandukuni hivyo kubobomoa kwa
kutumia
vyuma kisha kuchukuwa kiasi cha shilingi laki tisa na kutokomea
kusikojulikana.
Amesema kuwa baada ya kuona wameondoka yeye na
mke
wake walipiga yowe ambapo majirani walifika na kuwachukuwa hadi katika
kituo
cha polisi Musoma ambako walipewa fomu namba 3 na kisha kwenda kutibiwa
katika
hospital hiyo ambako amelazwa yeye na mke wake.
Akizungumzia tukio hilo kwa niaba ya kamanda
wa polisi
wa mkoa wa Mara,mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Mara Bw
Emanuel
Lukula amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa polisi bado
wanaendelea na uchunguzi.
