Wananchi wilayani Makete ambao hawajahesabiwa katika zoezi
la sensa ya watu na makazi lililoanza Agosti 26 mwaka huu wametakiwa kutoa
taarifa zao kwa wenyeviti wa vijiji ama vitongoji vyao ili waje kuhesabiwa
katika muda ulioongezwa na serikali
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete ambaye pia
ni mwenyekiti wa kamati ya sensa wilaya ya Makete wakati akizungumza kwenye
kikao cha kamati ya sensa wilaya ofisini kwake
Amesema katika kipindi hiki ambacho serikali imeongeza muda
wa kuhesabiwa hadi Septemba 8 ni vyema wananchi hao wakatoa taarifa kwa
viongozi wao wa vitongoji ama vijiji ili utaratibu wa kuwafuata walipo ili
wahesabiwe ufanyike mara moja
Amewataka wananchi hao kutosita kutoa taarifa hizo katika
kipindi hiki na kuwa muda hautaongezwa tena zaidi ya hapo
