MALORI YANAYOSOMBA PAMBA MKOANI MARA YAZUIWA

Wakulima wa zao la Pamba wa kjijiji cha Kihumbu katika kata ya Hunyari wilayani Bunda mkoani Mara,wamelazimika kuyazuia malori yanayosomba pamba kutoka katika maghala ya kijiji hicho kwa madai ya wanunuzi wake kushindwa kuwajalipwa fedha zao baada kuwazia pamba yao kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Wakisimulia mkasa huo kwa mbunge wa jimbo la Bunda Mh Stephen Wasira,wakati wa mkutano wa hadhara ambao umefanyikia kijijini hapo, wakulima hao wamesema wamelazimika kuchukua uamuzi huo baada ya kuhofia kuwa pamba yao ambayo wameyauzia makampuni hayo ingechukuliwa bila malipo.

Wamesema wamesema kabla ya kufikia hatua hiyo ya kuzuia magari ya kampuni hizo walipiga yowe na baada ya kukusanyika walifanya maandamano hadi kwene eneo la maghala hayo na kuanza kupanga mawe kwaajili ya kuzuia kuondoka kwa magari hayo.

Makampuni yanayodaiwa kununua pamba kwa mkopo kijijini hapo ni S&C
Ginneries,Olam(T) limited na Alliance Ginneries Ltd ambayo hata hivyo haijajulikana kiasi halisi cha fedha kinayodaiwa ingawa mwenyekiti wa
kijiji hicho Bw Kitenta Thomas, amesema zaidi ya wakulima 200  ndio wanaodai fedha hizo.
 
Kwa upande wake Mh Wasira ameonesha kusikitishwa na kitendo cha wanunuzi wa zao la pamba kuwakopa wakulima kinyume na maelekezo ya mkataba wa ununuzi na kuyataka yaache mara moja kufanya hivyo kwani ni kuvunja sheria huku akiwaasa wakulima kutokopesha mazao yao kwa namna yoyote ile.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo