MBUNGE AWAHAKIKISHIA WAFANYABIASHARA KUWA HAWATAONDOLEWA KATIKA SOKO LA MWIGOBERO MUSOMA

 
MUSOMA
 
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Mjini Vincent Nyerere amesema kuwa hakuna Mfanyabiashara yeyote atakayeondolewa katika eneo la Soko la Mwigobero bila kuonyeshwa sehemu nyingine ya kufanyia  biashara hiyo.
 
Akiongea kwa njia ya Simu kutoka Jijini Dar es Salaam,Mh Nyerere amesema kuwa zipo taarifa kuwa  Wafanyabiashara hao wanatakiwa kuondoka katika Eneo hilo la Soko la Mwigobero kupisha ujenzi wa soko la kisasa kwa ushirikiano na Mamlaka ya Bandari.
 
Amesema Wafanyabiashara wote waliopo katika eneo hilo hawataondoka eneo hilo bila kupewa eneo lingine,amesema Wafanyabiashara hao watapata Vibanda sehemu watakayotengewa hivyo waondoe  wasiwasi.
 
Naye Mstahiki Meya wa Manisspaa yaa Musoma Alex Kisurura  amesema kuwa tayari Mamlaka ya Bandari imetoa fidia kwa wafanyabiashara 46  walikuwa ndani ya soko hilo wakati wa Tathimini.
 
Kwasababu hiyo Mstahiki Meya  amesema kuwa wananchi wa eneo hilo la Mwigobero hawapaswi kuwa na hofu katika kufanyabiashara katika eneo hilo na hivyo kuwataka wafanyebiashara zao kwa amani.

Kauli za Viongozi hao zinafuatia malalamiko yaliyotolewa na Baadhi ya wafanyabiashara katika Soko hilo ambao walisema kuwa kumekuwepo na kutokuwa na Uwazi katika Mchakato wa Ujenzi wa Soko hilo huku Wafanyabiashara hao wakisema hawajui wapi watakapoenda kufanya biashara zao
 
Eneo la soko la Mwigobero linatarajiwa kujengwa kisasa kwa mujibu wa Viongozi hao ambapo Manispaa ya Musoma itashirikiana na Mamlaka ya Bandari kufanikisha Ujenzi huo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo