CHAMA cha waandishi wa habari mkoa wa Dodoma
(CPC)wamelaani vurugu zilizotokea
jana mkoani Iringa na kusababisha kifo cha mwandishi wa habari wa kituo cha utangazaji cha Chanel Ten
Daud Mwangosi.
Kauli hiyo
ilitolewa na Katibu wa chama hicho Habel Chidawali
alipokuwa akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari mkoani
hapa.
Chidawali amesema kuwa kamwe chama hicho
hakikubaliani na nguvu kubwa iliyotumiwa
na jeshi la polisi kwa ajili ya kumwaga damu ya mwandishi huyo ambaye hakuwa na hatia na kamwe jeshi la
polisi haliwezi
kujitetea
kwa kudai kifo cha mwandishi huyo ni bahati mbaya.
Amesema kuwajeshi la
polisi limekuwa likionyesha wazi wazi kuwa
linatumia nguvu,ubabe na matumizi mabovu ya silaha za moto
ambayo
hayajaweza kusaidia siku zote na badala yake
kinachoachwa ni maumivu
na vilio
kwa wananchi.
Katibu huyo
amesema kama jeshi la polisi linatuliza ghasia hakuna
siku hata moja haijatokea wakamuua kiongozi yoyote wa siasa
ambao ni
vinara wa
mikutano mbalimbali.
Kwa upande
wao wananchi mbalimbali mkoani hapa wamekemea nguvu kubwainayotumika na Polisi katika vurugu mbalimbali
zinazotokea.
Wamesema
tabia ya jeshi la polisi kutumia nguvu na silaha za moto
ambazo zinasababisha vifo vya watu wasiokuwa
na hatia.
Catheline Muhinte, amesema kuwa tukio
lililofanywa na jeshi la polisi
la kumuua
mwandishi wa habari linaonyesha dhairi kuwa kwa sasa jeshi
hilo linafanya kazi kwa kukiuka maadili ya
malengo yao.
Amesema
katika mwonekano wa picha ambazo zinaonekana katika vyombo mbalimbali vya habari inaonyesha dhairi kuwa polisi walihusika moja kwa moja na kifo cha mwandishi huyo.

