CUF YAWATAKA WANANCHI KUTOKUUZA MAZAO YOTE YA CHAKULA

Mwenyekiti wa Chama cha wananchi [CUF]Wilayani Siha Mkoani KilimanjaroBw Idd Amisi amewataka wananchi Wilayani humo  kutokuuza mazao yao yote ya chakula badala yake wajiwekee akiba ili kuepuka njaa
 
Akizungumza na waandishi wahabari wa Leo kwenye ofisi yake ,amesema imekuwa ni kawaida kwa wakulima katika wilaya hiyo kuuza mazao yote bil ya kujiwekea akiba ya kutosha jambo linalosababisha wakubwe na njaa
 
Bw Amisi amefafanuwa kuwa Wilaya hiyo ni moja ya Wilaya zinazozalisha mazao mengi ya chakula yakiwemo ,mahindi mihogo,viazi, na maharage, hivyo hakuna sababu ya kupata njaa kama ilivyo kwa maeneo mengine
 
Amesema kinachotakiwa kwa kila kaya kufahamu idadi yao iliwafahamu ni kiasi gani cha chakula kinatakiwa kuifadhi kama akiba
 
Ametahadharisha amesema wafanyabiashara wamekuwa na kawaida ya kuwarubuni wakulima hao wawahuzie mazao yote tabia hiyo wanapaswa kuiacha kwani inapelekea kuziacha familia nyingi kwenye matatizo ya njaa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo