MREMA ANG'AKA NA KNCU

 
Mbunge wa jimbo la Vunjo Agustine Mrema amemtaka mwenyekiti wa bodi ya KNCU Mernad Swai kuacha kupindisha ukweli kuhusu chama hicho na badala yake waungane katika kutafuta suluhu kuhusu deni la mabaki kwa wakulima.

Mh Mrema alisema kuwa amekuwa akifanya mikutano mbali mbali katika
jimbo lake akiwaelekeza wakulima wa zao la kahawa lakini amekuwa
akipingwa vikali na uongozi wa KNCU kwa kile walichodai ni uchochezi.

Aidha alisema kuwa KNCU walimfuata naibu waziri wa TAMISEMI Agrey
Mwanri ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Siha ili aweze kuwatetea
kuhusina na fidia ya mdororo wa uchumi lakini walishindwa na ilibidi
wamfuate.

“Walimfuata Mwanri na ikashindikana lakini mimi nikaona sio tatizo
ikanibidi niende kufautilia hilo deni la zaidi ya bilioni moja ila sasa wameniacha na wananipiga vita sasa nani nisaidiane naye katika
kuwasaidia wakulima hawa”alisema Mrema

Aliongeza kutokana na mdororo huo wa kiuchumi wa mwaka 2008/2009 KNCU ilitakiwa kufidiwa kiasi cha bilioni moja lakini  serikali kupitia
hazina ilishaijulisha KNCU kuwa haina fedhakwa ajili ya kuwalipa fidia.

Barua yenyekumbu na TYC/B/143/43 ambapo imeleza baada ya kupitia kwa kinaserikali haikuwa na fedha hii imepelekea KNCU kuwa katika hali mbaya kiuchumi na hatimaye kuwa na riba kubwa katika benki ya CRDB.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo