1. Chris
Cremence 100,000
2. Anonymous
500,000
3. Maggid
Mjengwa 100,000
4. Raymond Kasoyaga 20,000
5.Edward
Mgogo 10,000
6.Joachim
Kiula 5,000
7.Libory
Muhanga 5,000
8.Geofrey
Kagaruki 10,000
9.Sadiki Mangesho
10,000
10. Edwin
Namnauka 40,000
11.Daud Mbuba
10,000
12.
Anonymous 200,000
13.Mikidadi Waziri
6,000
14.
Bungaya Mayo 5,500
15. Abraham Siyovelwa
50,000
16.
Godfrey Chongolo 22,222
17. Jacob Mwamwene
51,000
18. Dennis
Bwimbo 153,683
Jumla:
1,298,000 ( Milioni Moja Na Laki Mbili Na Tisini Na Nane
Elfu Na Mia Tatu Na Themanini Na Tatu)
Kiasi kilichobaki kutimiza lengo? 900,000 ( Kiasi cha shilingi lakini tisa)
Kiasi kilichobaki kutimiza lengo? 900,000 ( Kiasi cha shilingi lakini tisa)
Background:
Ndugu zangu,
Daud
Mwangosi ambaye pia alikuwa 'Mwanakijiji' mwenzetu hapa Mjengwablog
hatunaye tena.
Nimemfahamu
Daud Mwangosi tangu mwaka 2004 nilipofika Iringa. Tangu wakati huo,
amekuwa akiinipa ushirikiano mkubwa kwenye kazi ya kutangaza shughuli
za kijamii kwenye Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi.
Ni kwa kupiga
picha za televisheni na kurusha habari kwenda Channel Ten; Iwe ni
kwenda naye Ilula au Njombe, Daud Mwangosi alikuwa tayari kila
nilipomwomba aongozane nami kwa shughuli ya kijamii.
Mara nyingi nilimkuta Daud ofisini kwake (
Picha ya kwanza juu) akichapa kazi na huku mkewe akimsaidia kazi
nyingine. Daud Mwangosi alikuwa mbunifu. Alikuwa ni mwenye kiu ya
kujifunza mambo mapya kwenye teknolojia ya habari na mawasiliano.
Najua Daud Mwangosi alikuwa na malengo ya
kuendeleza shughuli zake za ujasiriamali. Mbali ya mambo mengine,
alikuwa na Photocopy machine ya kumwongezea kipato ambayo iliharibika
mwaka jana. Akawa na ndoto ya kuwa na studio ndogo ya kupiga picha za
vipande ( Passport Size). Yote ni katika kumwongezea kipato kutunza
familia yake.
Leo Daud Mwangosi hayuko nasi. Ameacha
familia, mjane na watoto wanne; Itika Mwangosi ( Mjane) Nehemia
Mwangosi ( 17) Kidato cha Nne Malangali Sekondari, Hetzgovina
Mwangosi (12) Bathsheba Mwangosi (9) na Moria Mwangosi ( 2)
Namini Daud Mwangosi angependa shughuli
alizokuwa akizifanya ziendelee na zije kuwasaidia watoto wake pia.
Jana na leo nimewasiliana na mjane wa
marehemu Mwangosi ambaye bado yuko Tukuyu. Nikamwambia kuna '
Wanakijiji ' wa Mjengwablog walioguswa na msiba wa Mwangosi na
wangependa kutoa pole yao imsaidie katika kupata mwanzo kutoka hapa
alipo sasa. Mjane wa Mwangosi amefarijika sana kusikia habari hizo.
Kwa vile tayari ameahidiwa msaada wa
kusomeshewa watoto. Msaada anaouhitaji kwa sasa ni kupata photocopy
machine ( Used) na kodi ya pango la ofisi. Jumla yake kwa yote hayo
mawili haitazidi shilingi za Kitanzania milioni mbili na laki mbili.
Hivyo msaada anaouomba kwa wenye mapenzi mema ni shilingi 2, 200,000 (
Shilingi milioni mbili na laki mbili). Shughuli hizo zitamsaidia
kujikimu.
Kutokana na hali aliyo nayo sasa,
Mwenyekiti wenu napendekeza nichukue jukumu la kuratibu michango
hiyo. Shime tushirikiane kufanikisha hili ili tumsitiri mjane wa
mwenzetu Daud Mwangosi.
Napendekeza
ifikapo mwisho wa mwezi huu ( Septemba) tuwe tumefanikisha zoezi
hili kwa yeyote aliye nacho, hata kama ni shilingi elfu tano, ni
msaada mkubwa.
Mjengwablog bado tuna rekodi nzuri katika
kuchangishana kuwasaidia wenye kuhitaji. Itakumbukwa, huko nyuma,
kwa pamoja, tulifanikisha kukusanya michango ile ya watoto wa
Somalia na kuikabidhi UNICEF, Dar es Salaam. Ni zaidi ya shilingi
milioni mbili.
Tulifanikisha
mchango wa kusaidia ukarabati wa maktaba ya Kijamii kijijini Mahango,
Madibira. Zaidi ya shilingi milioni nne.
Sasa ni zamu ya kumchangia mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi.
Kinachohitajika ni milioni mbili na laki mbili.
Naam, kutoa ni moyo, usambe ni utajiri.
Mwenyekiti wenu na familia yangu naanza kwa kuchangia
shilingi laki moja.
Na kama kawaida, taarifa za waliochanga na
kiasi kilichopatikana kitawekwa kwenye blogu kwa kila mmoja kuona.
Namna ya kuwasilisha michango: Tumia
M-Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money au NMB Mobile. Kwa namba 0754 678
252, 0712 95 61 31, 0788 111 765 ( Kwa walio nje mnaweza kutuma kwa
Western Union, jina la mpokeaji- Maggid Mjengwa)
Natanguliza Shukrani.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
