WATU
watano wakazi wa kijiji cha Makilawa kata ya Minyughe wilayani Singida,
wamehukumiw na mahakama ya wilaya adhabu ya kutumikia jumla ya miaka 52,
baada
ya kupatikana na hatia ya kuvunja mlango wa duka la Jisaba Jaji, na
kisha kuiba
mali na fedha tasilimu, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni
2,168,000.
Washitakiwa
hao waliopewa adhabu hiyo ni Hasan Jumanne, Rashid Mwela Mwanga na Seif
Ismail
Nguru, ambao kila mmoja atatumikia jela miaka 14.
Washitakiwa
wengine ni Abdallah Masoud Iboma na Jumanne Mjoi@Banka. Hawa watatumika
jela
kila mmoja miaka 10.
Mapema
mwendesha mashitaka mwanasheria wa serikali, Mary Mdulungu, alidai mbele
ya
hakimu wa mahakama hiyo, Flora Ndale kuwa mnamo Julai 13 mwaka jana saa
4:30
usiku huko kijiji cha Makilawa, washitakiwa kwa makusudi walivunja
mlango wa
duka mali ya Jisaba Jaji, na kuiba mali mbali mbali na fedha taslimu
300,000/=.
Alisema
pamoja na fedha hizo taslimu, washtakiwa waliiba sola moja aina ya sujo,
simu
tano aina ya nokia, pea 85 za vitenge na pesa 104 za khanga.
Mdulungu
alitaja mali nyingine iliyoibwa ni katoni mbili za betri aina ya tiger
na
dazani mbili ya perfume mali yote hiyo pamoja na fedha taslimu shilingi
300,000, thamani yake ni shilingi milioni 2,168,000.
Kabla
ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mwanasheria wa serikali, Mdulungu, aliiomba
mahakama hiyo, itoe adhabu kali kwa washitakiwa ili iwe fundisho kwao na
kuogofya watu wengine wanaotarajia kutenda aina ya makosa ya wizi na
unyang’anyi.
Kwa
upande wao washitakiwa kila mmoja kwa nafasi yake, waliiomba mahakama
hiyo
iwape adhabu nafuu.
Wakati
huo huo, mahakama hiyo ilimwachia huru kasimu Ramadhani baada ya upande
wa
mashitaka kushindwa kumuunganisha na shitaka hilo.
